KAMANDA wa ngazi ya juu wa Kundi la Kigaidi la Al Qaeda, Mokhtar
Belmokhtar ameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na Jeshi la Marekani
nchini Libya.
Inasemekana kuwa, watu wengine kadhaa wameuawa wakati wa mashambulizi hayo.
Kwa upande wake, Wizara ya Ulinzi ya Marekani kupitia Makao Makuu ya
Jeshi la nchi hiyo (Pentagon) imedai kuhusika na mashambulizi hayo
wakikusudia kumlenga gaidi huyo (Mokhtar Belmokhtar) wa mtandao wa Al
Qaeda.
Kanali Steve Warren, msemaji wa Pentagon amesema kuwa, mashambulizi
hayo yalifanywa Jumamosi usiku na kwamba hivi sasa wanatathmini matokeo
ya oparesheni yao hiyo.
Blmokhtar anaaminika kuwa ndiye aliyeongoza shambulizi kubwa la
kigaidi katika kiwanda cha gesi nchini Algeria mwaka 2013, shambulzi
lililosababisha vifo vya watu 35 wakiwemo raia watatu wa Marekani.
No comments:
Post a Comment