TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars imeanza mazoezi jana kwenye Uwanja
wa Boko Veterani kujiandaa na mchezo wa marudiano kuwania kufuzu kwa
fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) dhidi ya Uganda wiki
ijayo, huku wachezaji wawili, Vincent Barnabas na Mudathir Yahya
wakiongezwa.
Stars inayonolewa na makocha wazawa, Charles Mkwasa na msaidizi wake
Hemed Morocco, itakuwa ikifanya mazoezi asubuhi na jioni uwanjani hapo
huku timu ikiweka kambi yake katika hoteli ya Kiromo mjini Bagamoyo.
Wachezaji wote walioitwa wameripoti kambini tangu juzi na jana
walifanya mazoezi asubuhi isipokuwa Aggrey Morris ambaye ni majeruhi na
nafasi yake imekuchukuliwa na Vicent Andrew (Mtibwa Sugar) na Jonas
Mkude aliyekwenda kufanya majaribio Afrika Kusini nafasi yake ikizibwa
na Mudathir Yahya (Azam FC).
Katika hatua nyingine, mshambuliaji Rashid Mandawa wa Kagera Sugar
ambaye ni mmoja kati ya wachezaji walioitwa kwa mara ya kwanza, amesema
amefurahishwa kuitwa kwenye kikosi hicho na kuanza mazoezi vyema.
Mchezaji huyo ni alikuwa mmoja wa wachezaji wengine waliojitokeza
jana kwenye kikosi cha timu ya taifa kilichoanza mazoezi jana katika
Uwanja wa Boko Veterani, Dar es Salaam.
Mandawa ambaye amehamia Mwadui FC ya Shinyanga akitokea Kagera Sugar
ya Missenyi, alisema kwa upande wake inampa moyo na kuwa ni hatua nzuri
ya kukuza kipaji chake na kuahidi kufanya makubwa zaidi.
No comments:
Post a Comment