BAADHI ya walimu wa shule za msingi na sekondari mkoani Rukwa wameelezea
umuhimu wa serikali kuanzisha mtaala wa mafunzo ya afya ya uzazi na
ujinsia kwa ajili ya wanafunzi wote nchini ili kuwezesha kuelewa
fursa sawa kwa mwanamke na mwanaume katika kushiriki uboreshaji wa afya
ya jamii na shughuli za kimaendeleo na kiuchumi
WALIMU hao kutoka katika halmashauri za wilaya za NKASI KALAMBO na
SUMBAWANGA wameiambia TBC kwa nyakati tofauti wakati wa maandalizi ya
kuukabidhi mradi wa mpango wa Afya ya uzazi na ujinsia-TMEP-kwa serikali
ya mkoa wa Rukwa, kuwa tofauti kubwa ya kupata haki za kimsingi kati ya
mwanamke na mwanaume inachangia kuzorota kwa shughuli za maendeleo
WAMESEMA kutolewa kwa elimu hiyo kwa wanafunzi wote nchini tofauti
na ilivyokuwa sasa kwa mikoa miwili ya mradi ya Rukwa na Singida
kutawawezesha wanafunzi hao kuepukana na mimba za utotoni sambamba na
kuelewa majukukumu sawa kwa mwanamke na mwanaume kwa ajili ya ustawi
bora wa jamii
No comments:
Post a Comment