Klabu ya Yanga imeshindwa kuonyesha makali yake baada ya kukubali
kipigo cha Magoli mawili kwa moja kutoka kwa klabu ya Gor mahia ya Nchni
kenya.
Katika mcehzo huo Yanga ilikua ya kwanza kupata goli kupitia
mshambuliaji wake Donald Ngoma katika dakika 4 ya kipindi cha kwanza.
Hali ya mchezo ilibadilika na Gor mahia walicheza kwa kasi
kuhakikisha wanasawazisha goli hilo na juhudi zao zilizaa Matunda baada
ya Mshambuliaji wao Harun Shakava kutingisha nyavu za Yanga katika
Dakika ya 18 kipindi cha kwanza.
Dakika ya 23 Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma alitolewa kwa Kadi
nyekundu na mwamuzi wa mchezo huo Ssali Mashood baada ya kumfanyia
madhambi Harun Shakava wa Gor Mahia.
Mpaka mapumziko timu hizo zilienda sare ya goli moja kwa moja ambapo
katika kipindi cha pili dakijka ya 61 Michaeli olunga aliipatia Gor
Mahia goli la pili,
Dakika ya 72 ya mchezo huo Nadir Haroub Canavaro alikosa penalti
No comments:
Post a Comment