Mwanafunzi
huyo mwenye umri wa miaka 21 (jina linahifadhiwa) anayesoma shahada ya
biashara, mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Acharya, Bangalore,
alifanyiwa ukatili huo akiwa na Watanzania wengine wanne.
Gazeti
la Deccan Chronical la Bangalore, liliripoti kuwa tukio hilo lilitokea
Januari 31, baada ya mwanafunzi raia wa Sudan, Ismail Mohammed kugonga
gari la raia mmoja wa India, mkazi wa Hesaraghatta aliyekuwa na mkewe na
kusababisha kifo cha mama huyo.
Nusu
saa baadaye, Watanzania watano akiwamo aliyevuliwa nguo, walifika
katika eneo hilo wakiwa kwenye gari ndipo kundi la watu hao lilipoanza
kumshambulia binti huyo, kisha kumvua nguo na kumlazimisha atembee uchi.
Baada ya kuchoma gari lililosababisha ajali hiyo, kundi hilo pia liliteketeza gari alilokuwamo Mtanzania huyo.
Msemaji
wa Wizara ya Mambo ya Nje, Mindi Kasiga alisema Balozi wa Tanzania
nchini humo, John Kijazi ameshakutana na wanafunzi hao na ameshazungumza
na Serikali ya India kuhusu tukio hilo.
Gazeti
la Deccan Chronical liliripoti kuwa licha ya polisi waliokuwapo eneo
hilo hawakuchukua hatua yoyote hata pale msamaria mwema aliyejitokeza
kumsitiri msichana huyo kwa fulana yake ambaye pia alipigwa huku fulana
hiyo ikichanwa.
Mshauri
wa masuala ya sheria kwa wanafunzi kutoka Afrika wanaosoma Bangalore,
Bosco Kaweesi alinukuliwa na gazeti la The Chronical akisema hata dereva
wa gari alilokuwa Mtanzania huyo, Micah Pundugu alipigwa na kujeruhiwa
vibaya.
Alisema hata pale msichana huyo alipojaribu kupanda basi ili kujinusuru na zahama hiyo, abiria walimshusha.
No comments:
Post a Comment