Rais John Pombe Magufuli akiwasili mkoani Arusha tayari kwa mkutano |
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasili
Mkoani Arusha ambako pamoja na mambo mengine ataongoza Mkutano wa 17 wa
kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
utakaofanyika Jumatano tarehe 02 Machi, 2016 Mjini Arusha.
Katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Rais Magufuli
amelakiwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali pamoja
na vikundi vya burudani za ngoma kabla ya kuelekea Arusha Mjini.
Rais
Magufuli ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
inayojumuisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.Kabla
ya kuongoza kikao hicho Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na kufanya
mazungumzo ya ana kwa ana na viongozi wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
Tarehe
03 Machi, 2016 Rais Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya, wataweka jiwe
la msingi katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Arusha - Holili -
Taveta - Voi inayoziunganisha nchi za Tanzania na Kenya.
Barabara hiyo ni sehemu ya miradi ya maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayotekelezwa na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.
No comments:
Post a Comment