Blatter akanusha kuhusika na rushwa
Rais wa FIFA Sepp Blatter amesema shrikisho hilo la kandanda duniani
linachukuwa hatua kuwaondoa hofu wafadhili, kuhusiana na kashfa za
rushwa, huku akikanusha kuwa aliidhinisha malipo ya dola milioni 10 kwa
mmoja wa maafisa waliokamatwa kwa tuhuma za rushwa - Jack Warner.
Blatter amesema katika mkutano wake wa kwanza na wandishi wa habari
baada ya kuchaguliwa tena kuiongoza FIFA hapo jana, kwamba atafanya
ziara binafsi ya kukutana na wafadhili wakuu wa FIFA walioeleza wasiwasi
wao. Miongoni mwa wafadhili wakuu walioleza wasiwasi kufuatia kadhia
hiyo ni pamoja na kampuni za Visa, Coca Cola, na ile ya vifaa vya
michezo ya Ujerumani Adidas. Blatter amesema walikuwa na mawasiliano na
wafadhili hao na wanaanza kurudisha heshima ya FIFA. Blatter amesema
kadhia ya Jack Warner haimhusu na kuongeza kuwa Wamarekani wana haki ya
kuchunguza madai hayo, lakini yeye hana wasiwasi wowote kwamba anaweza
kuhusishwa na kadhia hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment