CAR:Hatuna pesa za kutosha kuandaa uchaguzi

CAR:Hatuna pesa za kutosha kuandaa uchaguziSerikali ya mpito ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imesema kuwa inahitaji mamilioni ya dola ili kuweza kuandaa uchaguzi mkuu ujao. Rais wa serikali hiyo, Bi. Catherine Samba-Panza amesema hapo jana kuwa Jamhuri ya Afrika ya Kati inahitaji takriban dola milioni 17 ili kuweza kuandaa uchaguzi wa bunge na ule wa rais kwa wakati ufaao. Rais Catherine amesema hayo mjini Bangui wakati wa mkutano wa wafadhili wa uchaguzi ulioanza jana Jumanne. Umoja wa Ulaya ni moja kati ya wafadhili wakuu na wajumbe wake wako Bangui kuhudhuria kongamano hilo. Rais wa serikali ya mpito, Catherine Samba-Panza amezitaka nchi za dunia zilizotoa ahadi ya kuisaidia Jamhuri ya Afrika ya Kati zitekeleze ahadi zao ili shughuli ya uchaguzi iende kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa.
Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia kwenye machafuko ya kisiasa na kidini baada ya kupinduliwa dikteta wa zamani wa nchi hiyo, Francois Bozize, mwaka 2013.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved