Mwenyekiti wa chama cha kandanda cha Uingereza FA Greg Dyke, ametaka
rais wa shirikisho la kandanda duniani FIFA, Sepp Blatter aondolewe
katika nafasi hiyo, kufuatia kadhia kubwa ya rushwa iliyoukumba mchezo
huo.
Dyke amesema hakuna njia ya kurejesha imani kwa FIFA wakati Blatter
akiwa bado yupo, na kuonegeza kuwa lazima aondoke kwa kujiuzulu, kupitia
uchaguzi au watafute njia ya tatu. Shirikisho hilo la kandanda
limetumbukia katika mgogoro wakati likijiandaa kuchagua rais mpya,
likishtumiwa na serikali ya Marekani kwa uozo. Maafisa saba walikamatwa
katika uvamizi wa alfajiri kwenye hoteli ya kifahari mjini Zurich, na
kutuhumiwa kwa kuchukuwa zaidi ya dola milioni 150 katika hongo, huku
maafisa wengine 14 wa FIFA na watafuta masoko wakituhumiwa kwa shughuli
haramu, udanganyifu na usafirishaji haramu wa fedha. Blatter amekuwa
akishika usukani wa FIFA tangu mwaka 1998, na amenusurika na kashfa
kadhaa zikiwemo kuhusu madai ya rushwa, katika utoaji wa zabuni za
uenyeji wa mashindano ya kombe la dunia, kwa Urusi mwaka 2018 na Qatar
mwaka 2022.
No comments:
Post a Comment