BONDIA wa Thailand, Kitschai Singwacha anatarajiwa kutua leo Dar es
Salaam kupambana na Cheka katika pambano lisilo la ubingwa
litakalofanyika keshokutwa kwenye ukumbi wa Sabasaba.
Katibu Mkuu wa Chama cha Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST), Antony
Rutta alisema jana kuwa bondia huyo atatua leo mchana, na kesho kupima
uzito tayari kwa mpambano huo wa raundi 12.
Alisema tayari Francis Cheka ameshafika Dar es Salaam akitokea Morogoro, akiwa ameshafanya maandalizi ya kutosha.
“Cheka ameshafika leo (jana) akiwa tayari ameshafanya maandalizi kwa
asilimia 99, kwa hiyo ataendelea kujifua hapa Dar es Salaam hadi
Jumamosi ambapo ndio siku yenyewe,”alisema.
Pambano hilo litakuwa la kwanza tangu Cheka atoke jela hivyo kutoa
fursa kwa mashabiki wake kushuhudia kujipanga upya kwa bondia huyo wa
Morogoro.
Mabondia wengine watakaopanda ulingoni siku hiyo ni Kasim Ouma kutoka
Marekani ambaye atapigana na Mtanzania, Shaban Kaoneka, huku Mtanzania
mwingine, Cosmas Cheka akidundana na Mkenya, Fred Nyake.
No comments:
Post a Comment