UDSM yaanza mikakati ya kupunguza madini ya fluoride kwenye maji

Tokeo la picha la UDSM                                                   HUENDA wakazi wa mikoa ya Kaskazini wataondokana na matatizo yanayosababishwa na athari za wingi la madini ya fluoride katika maji endapo watafiti watafanikiwa kupunguza madini hayo katika maji.
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Idara yake ya Uhandisi na Rasilimaji imefanya utafiti juu ya matatizo yanayosababishwa na madini ya Fluoride. Lengo la utafiti huo ni kujaribu kupunguza madini ya fluoride katika maji kwa kutumia teknolojia mbalimbali, ikiwamo mifupa ya ng'ombe iliyochomwa na kuchanganya na udongo.
Mhandisi Godfrey Mbabay wa Idara ya Uhandisi Rasilimaji anasema wanachukua mifupa ya ng'ombe na kuichoma kwa kutumia viwango tofauti vya joto kisha kuisaga. Anasema wanatumia viwango tafauti vya joto ili kutafuta kiwango sahihi cha joto linaloweza kuondoa majini ya fluoride katika maji.
Wataalamu wakichapata kiwango cha joto kinachotakiwa wanatumia kifaa maalumu cha kuchujia maji hayo na kupimia unga huo wa mfupa ya ng'ombe tayari kwa matumizi. Utafiti huo unafanyika katika eneo la Arumeru, mkoani Arusha ambapo asilimia kubwa ya watu wameathirika kutokana na maji wanayotumia yenye fluoride nyingi.
Tatizo kubwa la fluoride linaathiri mifupa ambapo baadhi ya watoto huzaliwa vichwa vikubwa, matatizo ya ubongo, kuwa na meno yenye rangi na wengine hupinda mikono na miguu hivyo kusababisha watoto wengi kuwa na matege. Maeneo ya Kaskazini mwa Tanzania katika mikoa ya Arusha, Singida, Shinyanga, Kilimanjaro, Simiyu na Mara, ndio yanayoathiriwa zaidi na maji yenye wingi wa madini la fluoride na kusababisha wakazi wa mkoa huo kuwa na meno yenye rangi.
Anasema watafiti wa mwanzo walilazimika kutafiti mifupa wakagundua imeathirika kutokana na matumizi ya maji hayo. Baada ya wataalamu kubaini kuwa mifupa ya ng'ombe iliyochomwa inaweza kuondoa fluoride kwenye maji waliamua kuendelea kufanyia utafiti vitu vinavyoweza kuondoa wingi wa madini ya fluoride kwenye maji kwa kutumia vitu vinavyopatikana katika mazingira halisi.
Vitu vingine vinavyotumiwa katika utafiti huo ni udongo, mawe ya chokaa, udongo wa 'gypsum' na udongo wa mfinyanzi. Arumeru kuna kituo cha utafiti wa madini hayo cha Ngurdoto. Katika kituo hicho wanatengeneza hilo chujio na chokaa, halafu wananchi wananunua kwa bei ndogo kwa ajili ya matumizi.
Kwa upande wake Mhandisi Anaeli Ulomi anasema utafiti wa kwanza ulifanywa mwaka 1950 wakati wa serikali ya Uingereza. Waligundua tatizo la madini hayo. Waingereza hao waligundua tatizo hilo lipo katika eneo hilo la ukanda wa Kaskazini mwa Tanzania. "Utafiti wa kina ulionesha kuwa hayo madini yalisambaa sehemu kubwa kuanzia bonde la ufa mpaka kwenye nchi yetu.
Ilionekana kuwa kuna kiasi kikubwa cha athari ya watu walioathirika na fluoride," anasema. Kuanzia wakati huo watafiti mbalimbali walianza kuangalia athari zinazotokana na matumizi ya maji yenye madini ya fluoride. Ulomi anasema wataalamu wa Kitanzania pia walifanya utafiti na kubaini kuwa madini hayo yana athari kwa binadamu kwa kusababisha meno kuwa na rangi ya kahawia, mifupa kupinda na kichwa kuwa kikubwa.
Anasema kutokana na tatizo hilo kuwa kubwa walijitokeza watafiti mbalimbali kwa ajili ya kukabiliana na hilo, kikwazo kikubwa ni uhaba wa fedha. Anasisitiza madini hayo yanahitajika mwilini kwa ajili ya kuimarisha mifupa, misuli na mfumo wa damu kwenye mwili wa binadamu, yakiwa kwenye kiwango kizuri ambacho hakizidi miligramu 1.5 kwa lita moja ya maji.
Ripoti za tafiti mbalimbali zilizofanyika katika maeneo zinaonesha kuwa maji hayo yana miligramu nne hadi 20 kiasi ambacho ni kikubwa mno kwa matumizi ya binadamu. Anasema baada ya kufanya utafiti hizo kwa ushirikiano na Wizara ya Maji na kuona ukubwa wa tatizo lililopo. Serikali iliamua kuzuia matumizi ya visima vyenye maji yenye madini hayo.
Miaka ya nyuma aliyekuwa Mbunge wa Kishapu, Paul Makolo aliuliza serikali inachukua hatua gani kuhusu tatizo la fluoride kwenye maji ya visima, hali iliyosababisha usumbufu mkubwa wa upatikanaji wa maji ya kunywa kwa wakaaji wa mji huo, katika mji mdogo wa Maganzo, uliopo Kata ya Songwa.
Baada ya swali hilo, serikali ilijibu kuwa ni kweli miaka ya nyuma teknolojia ya kupunguza madini hayo ilikuwa ni tatizo, lakini kuna teknolojia ilipatikana ya kupunguza madini hayo ya ziada kwenye maji ambayo yalijaribiwa huko Arusha na wilaya ya Hanang na kuonekana inafaa.
Kwa maelezo ya serikali majaribio hayo yangefanywa mkoani Shinyanga kwa kipindi hicho kwa kutumia wataalamu hao na kipaumbele kitatolewa katika eneo hilo lenye tatizo ili wananchi wapate mbinu ya kupata maji safi na salama. Serikali ilisema majaribio yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na wataalamu wa wizara ya maji, yalionesha uwezo wa mafanikio ya kiteknolojia hiyo ya kupunguza madini hayo ya fluoride hadi viwango vinavyokubalika.
Ilionekana kuwa maji yenye fluoride kiwango cha miligramu 2.8 hadi 15.6 katika lita moja yalipotumiwa kwa muda wa miezi 12 ya majaribio, mtambo ulioweza kuchuja maji na kupunguza fluoride hadi miligramu 0.3 hadi 1.5 katika lita moja. Viwango vinavyokubalika na Shirika la Afya Duniani.
Maendeleo ya jamii yoyote kinategemea kuwepo kwa maji ya kutosha na yenye ubora unaotakiwa. Katika hali yake ya asili, maji ni sehemu ya mazingira ambapo wingi na ubora wake ndio unaosaidia katika kuamua jinsi maji yatakavyotumika. Upatikanaji wa maji safi na salama kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na usafi wa mazingira ni muhimu katika kulinda afya za wananchi.
Sehemu za Kaskazini na Kusini mwa nchi zenye miamba aina ya volkano ni nzuri kwa upatikanaji wa maji chini ya ardhi. Hata hivyo kwenye baadhi ya maeneo, maji chini ya ardhi yana chumvi nyingi na madini ya aina ya fluoride ambayo yanaathari kwa matumizi ya binadamu.
Serikali inaendelea kushughulikia changamoto zinazotokana na uhaba wa maji salama katika maeneo ya Kaskazini ili kuondoa athari zinazotokana na madini ya fluoride. Maji yanayofaa yanaendelea kupungua siku hadi siku kutokana na kuongezeka kwa mahitaji.
Hata hivyo katika kipindi cha miaka 15 iliyopita, mahitaji ya maji yameongezeka kwa kiwango kikubwa kutokana na ongezeko la watu nchini, ongezeko la uzalishaji mali katika sekta mbalimbali hususan kilimo cha umwagiliaji, uzalishaji umeme, uzalishaji viwandani, utalii, uchimbaji madini, ufugaji, uvuvi, matumizi kwa ajili ya usafi wa mazingira na mahitaji ya maji kwa ajili ya wanyamapori.
Upungufu wa maji unasababishwa na uharibifu wa mazingira, hali inayosababisha vyanzo vingi vya maji kukauka au kupungua. Pia, upungufu wa maji hutokana na ukosefu au upungufu wa mvua katika baadhi ya maeneo hapa nchini na matumizi mabaya ya maji hayo.
Upungufu huo wa maji unaathiri uzalishaji wa chakula na umeme na kusababisha uharibifu wa mazingira, hali inayoleta migogoro na ushindani wa kutumia maji miongoni mwa sekta mbalimbali za kijamii na zile za kiuchumi hivyo jamii inapaswa kutunza vyanzo vya maji ili kukabiliana na uhaba wa maji nchini.
UTEKELEZAJI wa upelekaji wa umeme katika vijiji kadhaa wilayani Magu umekamilika kwa asilimia 53, Bunge lilielezwa jana.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage alisema wateja wapatao 1,887 wanatarajiwa kuunganishwa umeme katika mradi huo utakaogharimu Sh bilioni 3.35.
Mwijage alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Magu, Dk Festus Limbu (CCM), aliyetaka kufahamu mradi wa kupeleka umeme kwenye vijiji vya Yichobela/ Kinango toka Irungu na Kabila toka Magu Mjini umefikia hatua gani.
Naibu Waziri alisema mradi wa kupeleka umeme katika vijiji vya Yichobela na Kinango kutokea Irungu unahusisha ujenzi wa njia ya umeme ya msongo wa kilovoti 33 umbali wa kilometa nane.
"Ujenzi wa njia ya umeme ya kilovoti 0.4 umbali wa kilometa saba na ufungaji wa transfoma tano. Mradi huu unatekelezwa na Mkandarasi Chico-CCC (BJ) JV Limited kwa ufadhili wa Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili," alieleza Naibu Waziri.
Alisema mpaka sasa ujenzi wa njia ya umeme ya msongo wa kilovoti 33 umekamilika kwa asilimia 100; kazi ya upimaji na michoro ya njia ya msongo wa kilovoti 0.4 imekamilika kwa asilimia 100 na mkandarasi ameshaleta nguzo zote na transfoma tano kumalizia kazi zilizosalia.
"Mradi wa umeme kutokea Magu Mjini kuelekea Kabila kupitia Itumbili, Kitongo, Sukuma Sekondari, Lumeji, Busalanga, Nhaya Sekondari, Nhaya Senta na Mwashepi unahusisha ujenzi wa njia ya umeme ya msongo wa kilovoti 33 umbali wa kilometa 28; ujenzi wa njia ya umeme ya msongo wa kilovoti 0.4 umbali wa kilometa 10 na ufungaji wa transfoma 18," alieleza Mwijage.(HABARI LEO)
DK
SERIKALI imesema baada ya kukamilisha ujenzi wa barabara zinazounganisha mikoa mbalimbali nchini, itashughulikia barabara za mkoa mmoja mmoja.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge alisema hayo jana wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Liwale, Faith Mitambo (CCM).
Lwenge alisema kwa sasa serikali imejikita katika kuhakikisha mikoa yote inaunganishwa kwa barabara za lami, na itakapokamilisha hilo, itazigeukia barabara za mkoa mmoja mmoja ili kuziweka katika hali bora.
Awali, akijibu swali la msingi la Mitambo, alisema barabara ya Liwale-Nanguruku ni barabara ya mkoa yenye urefu wa kilometa 230. Naibu Waziri alisema katika mwaka wa fedha 2012/13, barabara hiyo ilitengewa jumla ya Sh milioni 1,066.92 na katika mwaka wa 2013/14, jumla ya Sh milioni 1,782.69 zilitengwa kwa ajili ya matengenezo mbalimbali. "Aidha, kufuatia mvua kubwa zilizonyesha katika kipindi cha mwaka wa fedha 2013/14 uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara ulitokea na kusababisha uharibifu mkubwa. "Kutokana na hali hii, barabara hii iliidhinishiwa jumla ya Sh milioni 1,091.53 kutoka Mfuko wa Barabara kwa ajili ya matengenezo ya dharura na kurudisha mawasiliano yaliyokuwa yamekatika katika barabara hii," alisema Naibu Waziri.(HABARI LEO)
DK
bunge1
WANASIASA wameambiwa kuwa ubunge hautatokana na kiungo cha albino na kuachana na fikra hizo potofu.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Perreira Ame Silima amekiri bungeni kuwa ni kweli zipo taarifa kuwa baadhi ya wanasiasa wanahusishwa na imani potofu za kutumia viungo vya binadamu ili kupata madaraka.
"Ni kweli habari ziko zinazungumzwa kuwa wanasiasa fulani na zinaibuka wakati kama huu ambako kuna joto kali la Uchaguzi Mkuu," alisema Silima na kuongeza: "Ubunge hautatokana na kiungo cha albino."
Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (CCM), aliyesema vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi vinaeleza kuwa wapo wanasiasa wanaotumia viungo vya albino kusaka umaarufu.
"Vyombo hivi vya habari vya ndani na nje ya nchi vinaeleza kuwa wapo wanasiasa waokwenda kwa waganga na kutumia viungo vya albino kujitafutia umaarufu. Kwa nini serikali isiwabane waandishi hawa ili iwataje wanasiasa hao ili wasiohusika wasitiwe doa," alihoji mbunge huyo wa Rombo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani alisema serikali imekuwa ikifanya jitihada kubwa katika kukabiliana na tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu, na kuwa lazima jamii kuanzia ngazi ya familia ibadili fikra zao.
Alisema haiwezekani albino wauawe katika baadhi ya mikoa au eneo fulani tu la nchi, hivyo elimu inahitajika kwa watu husika na kuwa serikali itaendelea kuchukua hatua zikiwamo za kuielimisha jamii.
Aidha, alisema kifaa maalumu kitakachofungwa kwa albino ili kufuatilia mienendo yao, kinaendelea kufanyiwa kazi na serikali ili kufahamu kama teknolojia kinafanya kazi na pia kufahamu kama ni salama.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Jenista Mhagama, alisema serikali haijalidanganya Bunge kuhusu kifaa hicho, na kuwataka wabunge kuungana pamoja na serikali katika kukomesha mauaji hayo yanayolitia aibu Taifa.
Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Philipa Mturano (Chadema), Silima alisema mpaka sasa watu 15 wa mauaji ya albino, wamekamatwa, kufikishwa mahakamani na kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa.(HABARI LEO)
(KILONGE)
Mhe. Rais Kikwete akizungumza huku Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakimsikiliza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati akifungua rasmi Mkutano wa Nne wa Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi. Mkutano huo umefanyika katika Hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam ukiwa umebeba Kaulimbiu isemayo "Diplomasia ya Tanzania Kuelekea Dira ya Taifa 2025".
Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ya Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani)
Wajumbe wengine wakiwemo Wakuu wa Vitengo katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifutilia hotuba ya Mhe. Rais Kikwete.(VICTOR)
Read more...
TAASISI ya Kifedha ya Bayaport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo,imesema hata Watanzania wanaoishi mikoani wanaweza kutumia fursa ya kukopeshwa viwanja katika mradi wa Vikuruti, uliopo Kibaha, mkoani Pwani. Unaweza kuptata fomu hapa.
Afisa Mipango wa Wilaya ya Kibaha, Obed Katonge, akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya mikopo ya viwanja, uliyofanyika mwishoni mwa wiki, katika hoteli ya Serena.
Bonyeza hapa kupata fomu ya mkopo wa viwanja kutoka Bayport Financial Serviceshttp://www.kopabayport.co.tz/RESERVATION%20FORM.pdf
Kauli hiyo imetolewa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa taasisi hiyo, Ngula Cheyo, ikiwa ni siku chache baada ya kuzindua huduma ya mikopo ya viwanja katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, huku akisisitiza kwamba si lazima mkopaji wa viwanja hivyyo atoke Dar es Salaam au Kibaha.
Kicheko cha furaha. Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga, kulia akifurahia jambo na Meneja Masoko na Mawasiliaano wa Bayport Financial Services, jijini Dar es Salaam.
Habari; Watanzania wengi wanaoishi mikoani wamekuwa wakiulizia kama nao wana weza kukopeshwa viwanja hivyo,hivyo Bayport imeona itowe ufafanuzi huu. Kwamba ni ruhusa. Kilaa mtu anaweza kukopa.
Cheyo alisema kwamba huduma hiyo ni ya Watanzania wote, ndio maana wamesambaza fomu za kuomba mkopo wa viwanja katika matawi yao mbalimbali, bila kusahau wale wanaoweza kukopa kwa njia ya mtandao wawww.kopabayport.co.tz.(VICTOR)
Read more...
4
Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servcius Likwelile akiwaeleza Mawaziri wa Fedha kuhusu serikali ya Tanzania mipango yake hasa kwenye miundombinu. Kutoka kulia ni Waziri wa Fedha wa Rwanda Bw. Claver Gatete na kushoto kwake ni Mchumi Mkuu Rugwabiza Minega Leonard. ilivyonufaika na fedha za Benki ya Maendeleo katika kutekeleza.
3
Waziri wa Fedha wa Rwanda Mhe. Claver Gatete akitoa ufafanua wa masuala mbalimbali yanayohusu nchi za Afrika. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile ambaye amemwakilisha Waziri wa fedha na kulia kwake ni Waziri wa Fedha wa Ethiophia Mhe. Fisseha Aberra.
5
Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile akitoa ufafanuzi kuhusu Tanzania inavyoshirikiana na Benki ya Afrika kwa Mawaziri wa Fedha kutoka nchini Rwanda, Ethiophia, Kenya na Visiwa vya Shelisheli wakati wa uwasilishaji wa ripoti ya utekelezaji wa mazimio ambayo kila nchi imejiwekea.
1
Kamishna wa Fedha za Nje Bwana Ngosha Manyoga akiwa katika majadiliano yanayohusu ya ripoti ya utekelezaji wa mpango wa mafanikio katika nchi za Africa.(VICTOR)
150526152603_oshoala_premio_bbc_640x360_bbc_nocredit
Mshambuliaji wa Nigeria na timu ya Wanawake ya Liverpool, Asisat Oshoala ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya BBC ya mwanasoka bora wa mwaka.
Oshoala, mwenye umri wa miaka 20 ni mchezaji wa kwanza kushinda tuzo mpya kutoka BBC World Service,kwa kura zilizopigwa na wapenzi wa kandanda duniani.
Mwanadada huyu amemuangusha Veronica Boquete wa Uhispania na Nadine Kessler wa Ujerumani,Scot Kim Little na Marta wa Brazil.
"ninapenda kutoa shukrani zangu kwa BBC,mashabiki wangu duniani na kila mmoja aliyepiga kura" alisema.
Tuzo hii ni ya kwanza kufanyika na Shirika la utangazaji la kimataifa.
Oshoala, ambaye ni mchezaji mwenye umri mdogo kuliko wote kati ya wapinzani wake, alikuwa mfungaji bora na alipigiwa kura wakati wa michuano ya kombe la dunia la wachezaji wa umri wa chini ya miaka 20 nchini Canada kipindi cha majira ya joto kilichopita.
Jitihada zake ziliifikisha Nigeria katika hatua ya Fainali ambapo ilikutana na Ujerumani, ambapo Ujerumani ilipata ushindi mwembamba dhidi ya Nigeria.
Pia alitoa mchango mkubwa katika timu ya wanawake ya Nigeria katika kutwaa ushindi wa kombe la mabingwa Afrika kwa wanawake mwezi Oktoba.
Hatua hiyo imeiwezesha Nigeria kufuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia kwa wanawake nchini Canada inayoanza tarehe 6 mwezi Juni
CHANZO:BBC
IMECHOTWA KWENYE MTANDAO NA VICTOR SIMON
Waziri wa maliasili na Utalii, lazaro Nyalandu akimsikiliza waziri wa Ardhi na Maendeleo vijijini, Celso Coreia jana mjini Maputo kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kuhifadhi Pori la akiba la selous nchini Tanzania lililoungana na Hifadhi ya Nnyasa nchini Msumbiji ambapo mbali na uhifadhi watashirikiana kupambana na ujangili , utaalamu na vifaa.
Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akibadilishana hati za makubaliano ya kuhifadhi Pori la akiba la selous nchini Tanzania lililoungana na Hifadhi ya Nnyasa nchini Msumbiji na waziri wa Ardhi na Maendeleo vijijini Celso Coreia, ambapo mbali na uhifadhi watashirikiana kupambana na ujangili , utaalamu na vifaa, jana mjini Maputo Msumbiji.
Waziri wa Maliasii na Utalii, Lazaro Nyalandu na waziri wa Ardhi na Maendeleo vijijini wa Msumbiji Celso Coreia wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kuhifadhi Pori la akiba la selous nchini Tanzania lililoungana na Hifadhi ya Nnyasa nchini Msumbiji ambapo mbali na uhifadhi watashirikiana kupambana na ujangili, utaalamu na vifaa.(VICTOR)

PINDA ATEMBELEWA NA MTOTO ALBERT

unnamed
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na mtoto Albert Kanan wa darasa la tatu katika shule ya msingi ya Ilalangulu wilayani Mlele ambaye alikwenda nyumbani kwa Waziri Mkuu katika kijiji cha Kibaoni akiomba kupiga naye picha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.(VICTOR)
Ni dhahiri sasa kuwa hatua ya vikao vya juu vya CCM kuwafungulia makada wake waliokuwa wamefungiwa kwa kuanza kampeni mapema na kutangaza tarehe za kuanza kuchukua fomu, vimechochea harakati za kusaka urais na kuongeza urefu wa foleni ya wanaotaka kuelekea Ikulu kumrithi Rais Jakaya Kikwete.
Hayo yamejitokeza ndani ya siku nne baada ya uamuzi huo wa CCM kutangazwa mjini Dodoma na kuwafanya makada wake, kuanza kujitokeza hadharani wakiweka bayana tarehe za kutangaza nia hiyo.
WanaCCM waliojitokeza ni mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Makongoro Nyerere, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya na Mbunge wa Kuteuliwa, Profesa Sospeter Muhongo ambao kwa nyakati tofauti wamethibitisha kuwa wanatangaza nia hiyo wiki ijayo.(P.T)
Read more...

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved