Misaada ya ukandamizaji yamuumiza kichwa Kenyatta

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema wakati umefika kwa mataifa ya Afrika kukoma kutegemea misaada kutoka mataifa ya nje.
Kupitia  ujumbe alioutuma katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter, rais Kenyatta amesema misaada hiyo ya kigeni mara nyingi huwa na vikwazo na masharti ambayo yanakandamiza.
Ameongeza kusema kuwa hatma ya bara la afrika siku zijazo haipaswi kuwa mikononi mwa mataifa ya magharibi ambayo mara nyingi huweka maslahi yao kwanza.
Nchi  ya Kenya  ni moja ya nchi Barani Afrika  ambayo hutegemea mabilioni ya dola kila mwaka yanayotolewa na mataifa ya kigeni na katika bajeti yake.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved