JK atua Arusha, Kuongoza Maadhimisho siku ya Kimataifa ya Albino

Rais Kikwete mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA).
Rais Kikwete mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA).

Rais Jakaya Kikwete amewasili mkoani Arusha kuongoza maadhimisho ya siku ya kimataifa wa Albino yatakayofanyika leo.
Aidha, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Rais Kikwete amepokelewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Albino Tanzania Bwana Ernest Kimaya.
Watu wenye ulemavu wa Ngozi wana adhimisha siku yao huku wakiwa na changamoto  lukuki ikiwemo kuuawa na kukatwa viungo vyao kwa imani za kishirikina suala linalopelekea kuishi katika nchi yao wakiwa hawana amani ya kutosha.
Mtandao wa Hivisasa unaungana na Watanzania wote kuadhimisha siku ya Mataifa ya Albino huku tukiwataka wananchi  kuachana na imani potofu kwani mafanikio huletwa na juhudi zako katika kufanya kazi sio kwa kutegemea kiungo cha binadamu mwingine.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved