Urais 2015: Balozi Ali Abeid Karume kuvunja makundi CCM ?

Mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi ccm balozi ali abeid karume alipotangaz nia ya kugombea urais.
Mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi ccm balozi ali abeid karume alipotangaz nia ya kugombea urais.
Mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi ccm balozi ali abeid karume amesema kuwa endapo atapa ridhaa ya kuteuliwa kuwa Rais atahakikisha kuwa anayavunja makundi yote ya wagombea yaliyopo hivisasa.
Amesema hayo  wakati  akizungumza na wanachama wa CCM wilaya ya wete na kusisitiza kuwa anatambua kwamba kila mgombea anakundi lake. ameahidi kuwafuata na kushauriana na wanachama wenzake ambao wanamakundi hasa katika kipindi  hiki cha kinyanganyiro cha kuomba ridhaa ya chama kupitishwa kugombea nafasi ya urais.
“natambua kuwepo na makundi ya wagombea ndani ya chama , lakini iwapo mimi wataniamini nitahakikisha kwamba makundi ninayavunja na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ndani ya chama cha mapinduzi ambayo itawashirikisha wagombea wote walioingia kwenye mchakato hu ” amesema Karume
Akizungumzia mikakati yake akichaguliwa kuwa rais  amesema kuwa iwapo atapitishwa na chama chake kugombea nafasi hiyo atahakikisha kwamba anatenda haki na kubadilisha uchumi wa nchi kwa kuimarisha elimu ya ujasiriamali ili kuwafanya vijana kuweza kujiajiri wenyewe .
Hii ni mara ya pili kwa balozi ali abeid aman karume kuwania nafasi ya urais wa jamhuri ya muungano wa tanzania ambapo mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2005.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved