Fareed Kubanda aka Fid Q ana sababu za kwanini hana mpango wa kuwa mwanasiasa.
Akizungumza na New Day Taarifa jana, Fid Q alisema hapendi kuona wanasiasa jinsi wanavyobadilikika baada ya kupata pesa.
“Nimekutana na watu tofauti tofauti wanasema nafaa kutokana na uwezo
wangu wa kuchanganua mambo,” alisema. “Na siku moja nilijifunza kwamba
mapinduzi ni kitu ambacho kinaendelea, kila siku tunaimba malaria halafu
inakuja Dengue, mara tunaimba kuhusiana na mafuriko na mambo mengine.
Kwahiyo hivyo hivyo na huko serikalini vitu vipo hivyo, unaingia mule
ndani unakuta kuna mapengo kibao, kuna makorongo kibao, sasa unaamua
mwenyewe kama utaenda kuwa real au la!
Kule ukitaka kuwa mjuaji sana kuna matatizo yake pia na nachoogopa
mimi kuwa mwanasiasa ni kupata zile hela nyingi halafu nianze kuwa
muongo. Sio kama siasa inanishinda, napenda siasa lakini naogopa uongo.
Kama wanavyosemaga napenda umaarufu nachukia mbwembwe zake. Napenda
siasa nachukia uongo wake,” alifafanua rapper huyo.
“Kwa sababu kuna mdau mmoja alisema kwamba wanasiasa wote ni kama
unavyoona story ya binadamu wa kwanza. Kwamba binadamu wa kwanza alianza
kama sokwe halafu akawa binadamu. Siasa inaprove kinyume. Anakuja kama
binadamu halafu baadae anakuwa Sokwe.”
No comments:
Post a Comment