Diamond anawania vipengele vitatu ambavyo ni Best Male Act, Best Collaboration kupitia wimbo wake ‘Bum Bum’ aliomshirikisha Iyanya, na Best Live. Katika vipengele hivyo anachuana na Davido, Wizkid, Mr Flavour (Nigeria), AKA (Afrika Kusini) pamoja na Sarkodie (Ghana).
Tuzo za hizo zitatolewa Jumamosi ya July 18, 2015 huko Durban, Afrika Kusini na tukio hilo kuoneshwa moja kwa moja kupitia MTV Base (DStv channel 322), MTV (DStv channel 130) na BET (DStv channel 129) kuanzia saa 22:00 EAT.
No comments:
Post a Comment