SERIKALI imeendelea kuandaa mazingira ya sehemu itakayotumika kwa
ajili ya kumwapisha Rais mteule wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli.
Maandalizi ya mazingira hayo yanaenda sambamba na mazoezi ya kijeshi kwa
ajili ya gwaride maalumu, litakalofanyika wakati wa kuapishwa kwake
katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
HabariLeo lilifanikiwa kutembelea katika uwanja huo na kujionea jinsi
mazoezi hayo yanavyoendelea, ambapo mmoja wa askari jeshi aliyekuwa
akilinda eneo hilo alisema kinachoendelea ndani ya uwanja huo ni mazoezi
ya kijeshi kwa ajili ya siku hiyo.
“Mazoezi ya kijeshi na gwaride yanaendelea humu ndani, kwa sasa
wananchi wa kawaida hawaruhusiwi kuingia, ila siku husika ikifika
wataruhusiwa,” alisema mwanajeshi huyo. Dk Magufuli anatarajia kuapishwa
Novemba 5, mwaka huu baada ya kukamilika kwa taratibu zote za uchaguzi
na kukabidhiwa cheti cha ushindi.
No comments:
Post a Comment