Kikunizo Montage katika Moja ya Projects za Mashada Video Production |
Moja ya watayarishaji wakubwa wa Music Videos ndani ya Mbeya na nyanda za juu kusini,ambaye ni CEO wa Mashada Video Production,Kikunizo Montage amefunguka juu ya ujio mpya wa Mashada Video Production.Katika Interview aliyoifanya leo ndani ya Radio ya Bomba Fm 104.0,Alisema kwamba wamejipanga kutoa kazi zenye ubunifu zaidi kuliko zile za mwanzo.Pia Kikunizo Montage aligusia suala la gharama nafuu kwa 'upcoming artistes' ili kuwawezesha wafike mbali zaidi katika tasnia ya muziki.
Kikunizo Montage aliweka wazi kuanza kufanya kazi yeye mwenyewe tofauti na hapo mwanzo alipokuwa anafanya na Director mwenzake Friday Kyando "F2K" ambaye kwa sasa ameamua kufanya kazi mbali na Mashada Video Production.Kwa sasa Mashada Video Production inajihusisha pia na utengenezaji wa filamu ambapo kwa sasa karibia wanatoa filamu mpya inayoitwa DAMN TRICK.
Kaza buti brother..
ReplyDeleteAhsante...
ReplyDelete