Waislamu Russia wataka maeneo ya wanawake pwani
Pendekezo la jumuiya za Kiislamu nchini Russia kwa ajili ya kutengwa
maeneo ya wanawake na wanaume katika pwani za mito ya mji wa Moscow, kwa
ajili ya mapumziko, limeungwa mkono na viongozi wa dini nyingine nchini
humo. Albir Karganoff, naibu mkuu wa idara ya kidini kwa ajili ya
Waislamu wa Russia na mjumbe wa kamisheni ya uratibu wa mahusiano baina
ya makundi ya kidini na kaumu nchini humo, amesema kuwa tayari pendekezo
hilo limewasilishwa kwa viongozi wa serikali mjini Moscow. Amesema
kuwa, kuasisiwa maeneo hayo kutasaidia kuepusha uharibifu wa maadili
hususan kwa wanawake na wanaume wanaotembelea maeneo hayo. Karganoff
amesisitiza kuwa, kutengwa maeneo ya starehe baina ya wanawake na
wanaume ni jambo muhimu kwa wakazi hasa kwa kutilia maanani kwamba,
kunatoa uhuru kwa watu kufika maeneo hayo kinyume na ilivyo hivi sasa.
Aidha amesema baadhi ya nchi kama vile Uturuki na Ujerumani tayari
zimekwishaanzisha maeneo kama hayo kwa ajili ya usalama wa wanawake na
wanaume, suala ambalo limekuwa na taathira chanya kwa watumiaji.
Pendekezo hilo la Waislamu tayari limetiwa saini na kamati ya mahusiano
ya kijamii ya Kanisa la Orthodox nchini Russia na taasisi ya jumuiya ya
Mayahudi na Mabudha wa nchi hiyo, ambapo inatazamiwa kutiwa saini pia na
serikali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment