Kufuatia uteuzi wa wagombea nafasi za Ubunge na Uwakilishi kupitia
Chama cha Wananchi CUF ambao wamepitishwa na Baraza Kuu kumezua sokomoko
kubwa miongoni mwa wanachama na viongozi.
Jimboni Kojani hali sio shwari. Vipi linaanza kutimka baada ya
mgombea aliyeshinda kura za maoni kuekewa pembeni na kupitishwa mgombea
ambaye aliyepata ushindi wa pili. Jimbo la Kojani limejumuisha maeneo ya
Kisiwani Kojani na maeneo mengine ya juu. Kikawaida eneo la Kisiwani
hutoa Mwakilishi na eneo la juu hutoa Mbunge. Hayo ni makubaliano baina
yao. Nafasi ya uwakilishi inashikiliwa na Wakojani kindakindaki.
Yaliyoko ni Wakojani kugawika na kujipanga kupinga uteuzi wa
Uwakilishi wakidai Mteuliwa ambaye ni Mwakilishi kwa sasa hawafai kwani
hakufanya kitu katika miaka 5 iliyopita. Pia kashindwa kwenye kura za
maoni. Vilevile hakutowa ahadi zinazoeleweka nini atawafanyia miaka 5
ijayo. Alikuwa akitumia fedha zote za mfuko wa jimbo kwa maslah yake
binafsi. Yapo matawi 28 ndani ya jimbo la Kojani hakuna hata tawi moja
alilojenga. Ameshindwa kumaliza jengo la ofisi ya Jimbo la Kojani,
lililopelekea kusababisha kifo cha mtoto wa miaka 8 baada ya matufali
yake kumuangukia mtoto huyo. Kutumia fedha kutafuta kurudi tena kwenye
kiti. ripoti zote za Jimbo na Wilaya zilionyesha kutoridhishwa na
utendaji wake. Mwisho ni kuwa hakubaliki kwa Wakojani wenzake.
Kwa upande wa Mgombea aliyeshinda kura za maoni na hakupata kuteuliwa
yeye yuko juu kwa kukitumikia chama, pia ameonyesha CV zake za majukumu
aliyokuwa nayo. Ametowa ahadi za uhakikiwa ikiwa ni pamoja na kumaliza
jengo la ofisi ya Jimbo la Kojani. Kutumia fedha za mfuko wa jimbo kwa
kuwakabidhi wenyewe wananchi ili zitumike ipasavyo. Ameahidi kuchangia
chama ndani ya jimbo lake kwa kuwapatia mgao maalumu utakao saidia
kuendesha shughuli za chama jimboni hapo. Pia kumaliza matawi ya chama
yale yaliokwisha aanza kujengwa.
Kumetayarishwa Wakojani waliopo Unguja, Jimbo la Mtoni kwenda kumuona
Naibu Katibu Mkuu Mh Nassor Ahmed Mazrui na kumuelezea kadhia yao juu
ya uteuzi chama waliofanya. Timu nyengine ya Wakojani inafanya
inawasubiri Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Kuna baadh ya juhudi zimeanza kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na ofisi ya
Wilaya ya Wete kutakiwa kusuluhisha mzozo huu. Kiukweli moto unafukuta
na mwisho wake haujulikani wapii utaripuka.
No comments:
Post a Comment