Ishu za Viwanja vya Shule kunyang’anywa
na watu alafu wanafanyia shughuli nyingine badala ya kuweka viwanja vya
michezo ni moja ya vitu ambayo nimevisikia mara nyingi kwenye mijadala
ya Bunge.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikuwa Mwanza ambako alikuwa akifanya uzinduzi wa michezo ya UMISETA ambayo inafanyika Mwanza.
Kagusia ishu hiyo: “Michezo inahitajika sana katika jamii yetu.. Serikali lazima tuendelee kuhamasisha jamii itambue umuhimu wa Michezo.
Maeneo
mengi unakuta kuna migogoro ya maeneo ya Shule kuchukuliwa na watu
katika miji yetu, huu ni udhaifu kwa idara ya mipango miji hakuna sababu
ya hili kutokea.
Wakuu wa
Mikoa muhakikishe kila Shule na maeneo yake yanapimwa na yapewe hati ili
kulinda kwa ajili ya kuendeleza shughuli mbalimbali, tusipofanya hivyo
migogoro ya ardhi haitapungua hata kidogo“>>>– Waziri Mkuu Pinda.
No comments:
Post a Comment