Msanii huyo kutoka kundi la Maybach Music Group Rick Ross ameingia tena kwenye headlines safari hii baada ya kukamatwa na bangi aina ya Marijuana kwenye gari alilokua akitembelea masaa machache yaliopita.
Rapper huyo alisimamishwa na polisi huko Los Angeles baada ya polisi huyo kugundua kua vioo vya gari yake vilikuwa
vimepigwa tinted kinyume na matakwa ya kisheria, na baada ya
kusimamishwa alishusha vioo vya gari, ndipo Polisi huyo alipokutana na
harufu ya Marijuana na kukagua gari lake ndipo alipokutana na bangi hiyo kwenye gari.
Kwa sasa Rick Ross yuko chini ya ulinzi na anasubiri uhamisho wa kwenda jela iitwayo Georgia Fayette County Jail.
No comments:
Post a Comment