Jeshi la Polisi Kanda
Maalum Dar es Salaam limefanikiwa kukamata bunduki tatu katika matukio tofauti
jijini Dar esSalaam. Katika tukio la kwanza tarehe 12/06/2015 Polisi walipata
taarifa kuwa huko maeneo ya Mbagala Charambe (W) kipolisi Mbagala (M) Kipolisi
Temeke kuna majambazi wenye silaha wamepanga kufanya tukio la ujambazi katika
kampuni ya FM ABRI TRANSPORTERS iliyopo eneo ka Kurasini jijini Dar es Salaam
Polisi walikwenda
kuweka mtego na walipofika eneo la tukio majambazi yalianza kuwafyatulia risasi
nao walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi kisha kuwakamata watuhumiwa wawili
wenye silaha aina ya MARK IV yenye namba 308139 ikiwa na magazine yenye risasi sita. Bunduki nyingine ni SHORT
GUN yenye namba TZCAR 356460 ikiwa na risasi
saba ndani ya magazine. Bunduki zote hizi zimekatwa vitako na mitutu.
Aidha, zimekamatwa
pikipiki tatu eneo la tukio zenye namba T.769 CJW, MC.423 ASH, na MC.982 ASG
pamoja na simu za mkononi zipatazo nane za aina mbalimbali.
Katika
hatua ningine,
maeneo ya Pori la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mkabala na Mawasiliano Towers
(W) Kipolisi Oysterbay (M) Kipolisi Kinondoni, askari wakiwa doria walitilia
shaka mtu mmoja aliyekuwa pembezoni mwa pori hilo akiwa na pikipiki.
Walipomsogelea ili kumhoji, aliiacha
pikipiki na kutokomea porini. Askari waliikagua pikipiki yake namba MC. 406 AKF
Boxer rangi nyeusi. Pia waliipekua kwa kina na kufanikiwa kupata Bastola moja
nambari 152072 E yenye risasi tano
ndani ya magazine ikiwa imefichwa katika kiti (Seat) cha pikipiki hiyo.
No comments:
Post a Comment