Mwanaharakati Lastie Bone atoa album yenye kubadirisha mwelekeo wa Muziki Mbeya na Nyanda za juu Kusini

Kama wewe ni mfuatiliaji wa Muziki kamwe hutoweza kushangaa ukimsikia Lastie Bone,moja ya wanaharakati wa muziki wa kukomboa fikra za watu na producer maarufu wa muziki,Lastie Bone hatimaye ametoa album yake mpya hiitwayo SO SERIOUS.
Ndani ya Album hiyo kuna nyimbo 20 zilizo pikwa na Maproducer tofauti na wakubwa  nchini na mkoani Mbeya kama Gachi,Van Cigger,Burn Bob,Nach B,Lastie Bone,Da Most,Mensen Selekta,LilFrance na Ropper.
Nyimbo ndani ya album hii zimejaa kiwango kizuri na kusheheni mashairi yenye Punch Lines za kutosha mbali ya kuwa na ladha tofauti tofauti kukamilisha muziki wenye ufanisi,sanifu na kiwango cha kutosha.
Album hii inapatikana kwa mchango wa Sh.5000 PEKEE.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved