Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akilakiwa na Mbunge wa Muleba Kusini, Anna Tibaijuka, baada ya kuwasili kwenye Kijiji cha Kyamkwikwi, wilayani Muleba mkoani Kagera jana, kabla ya kupanda boti kwenda Kisiwa cha Bumbile wilayani humo wakati wa ziara ya Kanda ya Ziwa. Picha na Ofisi ya CCM |
Hali hiyo ilijitokeza jana asubuhi katika Kata ya
Nshamba wilayani hapa wakati msafara wa Kinana ulipofika kuzindua mradi
wa maji. Kadhia hiyo ilianza baada ya Katibu wa CCM Mkoa wa Kagera, Ally
Idd Ame kumkaribisha mbunge huyo ili awasalimie wananchi. Hata hivyo,
wananchi hao walianza kuzomea kwa zaidi ya sekunde 40 wakipinga Profesa
Tibaijuka kupanda jukwaani, hali iliyomlazimu Mkuu wa Wilaya, Francis
Isack kupanda jukwaani na kutoa kauli ya kiutawala ili kuwanyamazisha
wananchi hao.
“Anayetaka kusikiliza abaki na asiyetaka aondoke,”
alisema Isack na kuwanyamazisha mamia ya wananchi hao. Baada ya kauli
hiyo wananchi walitulia na kuruhusu Profesa Tibaijuka kupanda na
kuhutubia kwa muda.
“Kama hamnitaki siyo lazima niwe mbunge wenu,
mnaruhusiwa kubadili. Huyo aliyewapa viroba asubuhi hii ili mje mnitie
aibu mbele ya katibu mkuu wa chama nawaambia hiyo dhambi itawatafuna,”
alisema.
Aliwaambia wananchi hao kuwa anachokifanya ni kuwatumikia na kuwaletea maendeleo, hasa wanawake...
“Mimi sitafuti kazi na wala sina njaa... na kama
hela ya kula ninayo. Mimi sigangi njaa na kama mnataka kuwa na kiongozi
mganga njaa muwekeni muone atawasaidia vipi,” alisema.
Akihitimisha salamu zake kwa wananchi hao alisema
kama wana jambo lao la ziada walifanye lakini wamuache aendelee na
jitihada za kuwaletea wanawake maji... “Sina kinyongo na yeyote kwa
sababu “I am too sophisticated (mstaarabu). Nipo juu ya mambo
madogomadogo yanayowasumbua.”
Mbunge huyo ambaye hivi karibuni aliondolewa
uwaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutokana na kashfa ya
Tegeta Escrow, alimweleza Kinana kuwa eneo hilo limekumbwa na upinzani
kutoka kwa mtu anayehitaji kulichukua ambaye ni kutoka ndani ya CCM.
Profesa Tibaijuka alisema katika ubunge wake
amefufua mradi huo wa maji utakaogharimu Sh200 milioni kupitia shirika
moja ambalo mkandarasi wake ni wa Umoja wa Mataifa na utekelezaji
umeanza miezi minne iliyopita lakini unahujumiwa.
“Mradi huu wa Nshamba unahujumiwa na wapinzani
wangu kutoka ndani ya CCM na vyama rafiki vya kisiasa, lakini lengo lao
ni kunidhoofisha kisiasa, jambo ambalo linadidimiza maendeleo,” alisema
Profesa Tibaijuka ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Makazi la
Umoja wa Mataifa (UN – Habitat).
Kinana na kahawa
Katika ziara hiyo, Kinana aliitaka Serikali mkoani
Kagera kusimamia wakulima kuuza kahawa ndani na nje ya nchi ili
wanufaike badala ya kuwahusisha na magendo.
No comments:
Post a Comment