Mhe. Anne Kilango Malecela |
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Anne Kilango Malecela (Mb) alipokuwa akijibu swali kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bungeni leo.
Katika swali lake, Mhe. Rita Kabati (Mb) alitaka kujua ni shule ngapi na vyuo vya Elimu hapa nchini ambavyo vimeruhusiwa kutoza ada kwa fedha za kigeni
Mhe. Malecela amesema serikali haijawahi kutoa kibali cha kutoza ada kwa fedha za kigeni kwa shule au vyuo isipokuwa kwa shule zile zilizoanzishwa kwa ajili ya kuhudumia watoto wa mabalozi, maofisa wa ubalozi na wanafanyakazi kutoka mataifa ya nje walioko nchini, ambazo hutumia mtaala wa kimataifa na kutoza ada kwa fedha za kigeni.
Amezitaja shule zinazotoza ada kwa fedha za kigeni kuwa ni Dar es salaam Internationa School, International school of Tanganyika, Haven of Peace International School na Laureate International school and educationa Trust Fund.
Mhe. Malecela amesema kuwa nyaraka na miongozo ya elimu iliyowahi kutolewa na Kamishna wa Elimu kwa lengo la kusimamai utekelezaji wa sera ya elimu haijawahi kutoa kibali cha kutoza ada kwa fedha za kigeni.
Amesema hata waraka wa elimu Na. 10 wa mwaka 1998 unaohusu “mabadiliko ya ada kwa shule na vyuo vya ualimu vya binafsi na walaka wa elimu Na. 19 wa mwaka 2012 unaohusu “ongezeko la ada kwa shule zisizo za serikali” zilitoa viwango vya ada kwa shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu vya binafsi kwa fedha za kitanzania kuzingatia kuwa utoaji wa elimu ni huduma na si biashara.
Amesema kuwa hata utozaji wa ada katika vyuo Vikuu unaodhibitiwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), viwango vya ada vinavyotakiwa kutozwa ni kwa fedha za kitanzania tu. Lengo ni kumuwezesha kila mtanzania kupata elimu stahiki bila kikwazo.
No comments:
Post a Comment