Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta |
Sitta alisema hayo jana wakati akizungumza na
makada wa chama hicho waliojitokeza kumdhamini katika wilaya ya Geita
mkoani Geita na kusema kuna baadhi ya watia nia wanaopita wakisema kuwa
wakiwa marais watapambana na rushwa wakati ukiwatazama macho yao
yanaonyesha ni wala rushwa. Viwango vya kubadili fedha za kigeni, kwa
sasa Dola moja ya Marekani sawa na Sh2,000.
“Nilitumwa Canada kutafuta ndege tatu, jioni moja
tukiwa Canada tunajiandaa kuondoka, akaja mkurugenzi wa masoko wa
kampuni tuliyonunua ndege, akaniambia waziri tuna kautaratibu hapa
ukifanikisha ndege zetu zikanunuliwa tunatoa bakshishi ya Dola 70,000
utataka hizi hela tuzipeleke benki gani,” alisema Sitta akimnukuu ofisa
huyo wa masoko.
“Watazameni hawa watu... mtu kawa waziri mwaka
mmoja leo anataka urais, halafu anasema atapambana na rushwa…utapambana
na rushwa wapi wakati hata hujapita kwenye mitego ya rushwa. Watazameni
kwa makini, mtawajua tu kwa macho, kwani macho yao yamekaa kijanjajanja
kweli,” alisema. Aliendelea, “Kwa kuwa mimi nililelewa vizuri nilijua tu
huo ni mtego wa shetani, nikamwambia mkurugenzi nitampa jibu kesho,
nikawasiliana na wakubwa zangu kwanza wakakubali ni chukue hiyo pesa
ikasomeshe marubani wa ndege.”
Sitta aliwataka wananchi hao kuwatazama kwa makini
watangaza nia hao, na kuwauliza iwapo tayari walishawahi kupambanishwa
na rushwa.
Lowassa aonya kuhusu viongozi wanafiki
Kigoma. Wakazi wa Kigoma wametakiwa kuwa makini na
kauli za baadhi ya viongozi wa Serikali wanaojinadi kwa kusema
wanawapenda Watanzania maskini, lakini mioyoni mwao hawana huruma.
Hayo yalisemwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa alipokuwa akitafuta wadhamini
mkoani hapa, muda mfupi baada ya kukabidhiwa fomu zenye majina ya wanachama waliojitokeza kumdhamini.
Akiwa katika ofisi ya CCM mkoa, Katibu wa CCM
Wilaya ya Kigoma Mjini, Nohoji Kubaji alimkabidhi Lowassa fomu 45 za
wana CCM waliomdhamini.
“Wapo viongozi, wanajifanya wanawapenda na
kuwajali watu masikini, lakini wao wenyewe unawakuta ni matajiri, hawa
jamaa ni waongo sana hawa,” alisema.
Lowassa aliwataka wakazi Kigoma kumuombea ili dua
na sala zao ziweze kumsaidia afikie malengo aliyojiwekea. “Nina dhamira
ya kuwatumikia, lakini lazima mniombee sana dua na sala ili mambo yangu
yaende vizuri hatimaye nishinde kuwa Rais wa Tanzania. Mimi nachukia
sana umaskini, kwa hiyo lazima tuwe kama Malaysia ambayo kiongozi wake
alipambana kuhakikisha wananchi wanaondokana na umaskini,” alisema.
No comments:
Post a Comment