Maalim Seif, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar, aliwataka vijana popote walipo kujiandikisha kwa ajili
ya uchaguzi ili kujitayarisha na ushindi aliouita mkubwa.
Alitoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye Viwanja vya Tibirinzi, Chake Chake Pemba na
kuhudhuriwa na maelfu ya wafuasi wa chama hicho kikuu cha upinzani
visiwani Zanzibar.
“Hakuna kushindwa CUF, kwa hivyo mawazo yenu yawe
na kushinda tu. Vijana, hakuna kukaa ukasema ushamaliza kupiga kura,
unakwenda kwako unasubiri ushindi. Hakuna hilo mwaka huu, lazima
mjitahidi kulinda ushindi wenu,” alisema Maalim Seif.
Katibu huyo wa CUF alisema wananchi wa Pemba
walioko Arusha, Mwanza na sehemu nyingine warudi kujiandikisha kwenye
Daftari la Wapigakura na kuwataka kutoacha fursa hiyo ambayo ni haki yao
ya kidemokrasia.
Akitilia mkazo suala hilo, aliyekuwa waziri wa
SMZ, Mansoor Yussuf Himid alimtaka Maalim Seif baada ya kupiga kura yake
kurudi nyumbani na kuwaachia vijana kumkabidhi ushindi wa chama hicho.
Mansoor ambaye ni mshauri wa Maalim Seif, alisema
vijana wasitarajie kuletewa ushindi katika kisahani cha chai, washiriki
kikamilifu katika kupatikana ushindi wa chama hicho.
Mansoor alisema hatima ya ushindi wa Zanzibar ipo
mikononi mwa vijana, hivyo wanapaswa kuhakikisha ushindi wa Zanzibar
unapatikana katika ya mikono yao.
Akihutubia mkutano huo, Mwanasiasa Hassan Nassor
Moyo alisema kazi ya Maalim Seif na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Amani
Abeid Karume kuleta umoja wa kitaifa si jambo jipya kwa kuwa lilianzia
kwa Mzee Karume ambaye alitunga sheria kuondosha ubaguzi na kuwaweka
wananchi wote wa Zanzibar kuwa kitu kimoja.
Uchumi
Katika hotuba yake ya takriban saa moja
iliyorushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Star TV, Maalim
Seif alisema Maalim Seif alisisitiza nia yake ya kuifanya Zanzibar kuwa
na mamlaka kamili ili iondokane na adhabu ambazo siyo stahiki kwake.
Seif alisema Wazanzibari wamekuwa wakiadhibiwa kutokana na ufisadi unaofanywa na baadhi ya viongozi wa Bara.
No comments:
Post a Comment