Uvuvi wa bahari kuu wapigiwa debe

http://www.bungemaalum.go.tz/files/members/0cfeefba482ca636d7cf88febe964b1a.jpg
Amina Iddi Mabrouk
   KAMATI ya Uvuvi Mifugo na Utalii ya Baraza la Wawakilishi imeitaka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuharakisha kuanzisha Uvuvi wa Bahari Kuu ambao utasaidia kuongeza mapato kwa wananchi na taifa kwa kuvuna rasilimali iliopo.
Akisoma maoni ya Kamati ya Uvuvi Mifugo na Utalii hapo katika Baraza la Wawakilishi, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Amina Iddi Mabrouk alisema njia pekee ambayo itaiwezesha Serikali kuingiza mapato zaidi na wakulima kufaidika na sekta ya uvuvi ni kuanzisha uvuvi wa bahari kuu.
Alisema suala la kuanzisha uvuvi wa bahari kuu hivi sasa umekuwa wimbo wa Wizara katika bajeti zake mbalimbali lakini hakuna utekelezaji wake ambao utaleta tija kwa wananchi.
“Tunaiomba Serikali kuharakisha mikakati ya kuanzisha uvuvi wa bahari kuu kwani huko ndiko zilipo rasilimali ambazo wavuvi wanaweza kuvuna na kupata kipato,” alisema.
Aidha, kamati imeitaka wizara kuimarisha sekta ya mifugo ambayo imezorota sana huku wafugaji wakikosa mbinu na utaalamu wa kutunza mifugo.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved