Watu walioshuhudia wamesema mtu aliyekuwa na mabomu aliingia kanisa hapo katika eneo la Jigawa katika jimbo la Yobe na kuua watu wote watano waliokuwa wakifanya ibada ndani ya kanisa hilo. Watu wanne walikufa papo hapo na mwingine wa tano waliaga dunia baadaye akiwa hospitalini.
Wahanga wa mlipuho huo ni pamoja na pasta mmoja, mwanamke na watoto wake wawili na bwana mwingine mmoja.
Hadi sasa hakuna kundi lililotangaza kuhusika ya shambulizi hilo la kigaidi lakini mji wa Potiskum umekuwa ukilengwa kwa mashambulizi ya mara kwa mara ya kundi la Boko Haram.
No comments:
Post a Comment