AMIRI Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Kikwete
amekagua gwaride rasmi lililoandaliwa na vikosi mbalimbali vya jeshi
katika sherehe za jeshi hilo ambazo pia zilitumika kumuaga rasmi.
Katika sherehe hizo ambazo zilifanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini
Dar es Salaam jana, walihudhuria wageni mbalimbali. Ndege za kijeshi
zipatazo 25 zilipita angani katika uwanja huo kutoa heshima kwa Amiri
Jeshi Mkuu huyo ambaye anamaliza muda wa uongozi wake baada ya uchaguzi
mkuu, mwezi ujao.
Kikosi cha Makomando wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi (JWTZ) kilionesha
uhodari na ujasiri mbele ya Rais Kikwete. Majeshi hayo ya Ulinzi na
Usalama ambayo ni pamoja na JWTZ, Jeshi la Magereza, Jeshi la Polisi
Jeshi la Wanaanga, Wanamaji walitoa burudani ikiwa ni pamoja na nyimbo
kutoka makundi ya sanaa.
Kwenye sherehe hizo za kumuaga Rais Kikwete ambaye hakuzungumza zaidi
ya kushuhudia burudani, zilizofanyika sambamba na maadhimisho ya
kuzaliwa kwa JWTZ, Septemba Mosi, 1964.
No comments:
Post a Comment