Lastie Bone kahusika pia
Kati yao yupo dogo wa miaka 17
Wasafiri hadi Mbeya Mjini kutafuta Studio
Kenny Eyes,moja ya wasanii mahili wa Chunya |
Kutokana na kukua kwa tasnia ya muziki wa kizazi kipya ndani ya mkoa wa Mbeya na Nyanda za juu kusini,ushirikiano katika kuwasilisha ladha tofauti unaonekana kuleta chachu.
Jambo hilo limewafanya vijana kadhaa wanowakilisha wilaya ya Chunya kujikusanya na kutoa wimbo wa pamoja."Ilitubidi tusafiri hadi Mbeya mjini ili kufanya wimbo wenye kiwango kizuri"Aliongea Kasu,mmoja ya wasanii hao."Binafsi namkubali sana Lastie Bone na ndiyo maana nikakubaliana na swala la kumuweka yeye kuwa 'producer' wa wimbo,na kweli hakautendea haki"aliongezea Kenny Eyes.
Ndani ya wimbo huu,wasanii hawa wameelezea swala la watu kuleta dharau kutokana na kumchukulia mtu kutokana na wanavyomuona.Wimbo huuu umeitwa "Usilete Madharau".
"Kabla ya jina hili,tuliuita 'Kabla hujania',lakini kutokana na ujumbe mkubwa uliopo ndani yake,nikapendekeza uitwe 'usilete madharau' na wasanii wakakubaliana nam"Aliongea Lastie Bone,'producer' wa wimbo huo.
Sikiliza na kuupakua wimbo huo HAPA
No comments:
Post a Comment