Chama cha ACT Wazalendo kimemsimamisha uanachama Ofisa Mipango wake, Ali
Makame Issa kwa madai ya kukiuka maadili ya chama hicho.
Hata hivyo, Issa alisema jana kuwa hajapokea taarifa yoyote kutoka katika chama hicho.
Hatua
hiyo dhidi ya kiongozi huyo mwandamizi ndani ya ACT, imekuja baada ya
chama hicho kudai kuwa alishirikiana na aliyekuwa mgombea wa urais wa
Zanzibar, Khamis Iddi Lila kuwahujumu.
Awali, Lila alisimamishwa
uanachama kwa madai ya kutoa misimamo ya kushiriki uchaguzi wa marudio
uliotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha
Salim Jecha.
Barua ya ACT, iliyosainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa
chama hicho, Juma Said Sanani imesema: “Kamati maalumu ya Zanzibar
imekusimamisha rasmi uanachama kwa mujibu wa katiba ya ACT Ibara ya 11
(2) kuanzia leo Februari 19, 2016, kwa ukiukwaji mkubwa wa
katiba Ibara ya 7 (3)(5)(9) Ibara ya 10 (2)(c) (d), Ibara ya 22 (1) (2)
(4).”
Barua hiyo inabainisha kuwa mwanachama huyo amekiuka kanuni na maadili pamoja na kukidhalilisha chama.
“Huku
ni kukiingiza chama katika mgogoro kwa kuandika barua ya kushiriki
uchaguzi wa marudio na kuhudhuria katika kikao cha Tume ya Uchaguzi
Februari 17 ukijua kuwa chama kimeshapeleka barua Febuari 9 ya
kutoshiriki uchaguzi,” inaeleza.
Vyama vilivyowachukulia hatua
viongozi wake kwa madai ya kukiuka kanuni ni Sauti ya Umma (SAU),
kilichomfukuza aliyekuwa mgombea wake wa urais wa Zanzibar, Issa Mohamed
Zonga, huku Alliance for Democratic Changes (ADC) kikimfukuza aliyekuwa
mlezi wake, Hamad Rashid Mohamed
No comments:
Post a Comment