Kamanda mkuu wa polisi Morogoro Leonard Paul |
Watu watatu wamekamatwa na polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za kuvamia
Kituo cha Polisi cha Duthumi na kuvunja mlango kwa lengo la kuwatoa
wenzao watatu wanaotuhumiwa kwa wizi wa mifugo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Graifton Mushi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 12.40 jioni.
Alisema polisi walilazimika kutumia silaha za moto na mabomu ya machozi kuwatawanya watu hao.
Mushi
alitaja silaha hizo kuwa ni mapanga, shoka na marungu. Hata hivyo,
alisema wakati watu hao wanavamia kituo hicho watuhumiwa hao
walishaondolewa kituoni hapo na kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi
Kati. Alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya
uchunguzi kukamilika.
Katika tukio jingine; watu zaidi ya 20 wa
Kitongoji cha Mazizini Kijiji cha Maseye Wilaya ya Morogoro wamevamia
eneo la mwekezaji Ayubu Mngimbwa na kuteketeza vibanda vilivyokuwa na
vifaa mbalimbali vya uchimbaji wa madini na kumshambulia kwa vipigo.
Kaimu Kamanda huyo alisema thamani ya vibanda na vifaa vilivyoteketezwa bado haijafahamika.
No comments:
Post a Comment