Mkataba wa mchezaji huyo unamalizika mwisho wa msimu na hajapewa mkataba mpya.
Beki huyo wa umri wa miaka 35, aliyejiunga na klabu hiyo akiwa na umri wa miaka 14, ameshinda Ligi ya Premia mara nne, Kombe la FA mara tano na Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara moja akiwa na The Blues.
"Ningependa sana kuendelea kukaa, lakini klabu inaelekea upande tofauti,” amesema.
Terry amechezea Chelsea mara 696 na anatumai kuendelea kucheza, ingawa si katika klabu nyingine Uingereza.
"Walisema kwamba meneja mpya akija, mambo huenda yakabadilika,” Terry alisema baada ya klabu hiyo kulaza MK Dons 5-1 katika raundi ya nne Kombe la FA.
“Kwa sasa sijapata mkataba. Nilitaka kujua sasa kama ilivyokuwa awali kila Januari na hili huchukua miezi kadha kukamilishwa. Hautakuwa mwisho nilioutarajia. Sitastaafu soka nikiwa Chelsea, imechukua siku kadha kukubali hili.”
 
Baadaye hata hivyo, msemaji wa klabu alisema huenda Terry akapewa mkataba mpya.
"John ameshauriwa kwamba ingawa kwa sasa hajapewa mkataba wowote, kwamba hali inaweza kubadilika miezi kadha ijayo,” msemaji wa klabu hiyo alisema baadaye Jumapili.
“Klabu hii inamheshimu sana John na kuthamini yote ambayo ametusaidia kutimiza kufikia sasa.”

WHO yahofu virusi vya Zika kusambaa kwa kasi

Wataalam wa maswala ya afya wa shirika la Afya duniani WHO wanahofu kuwa virusi vinasambaa mbali na kwa haraka,vikisababisha madhara makubwa.
maambukizi yamekuwa yakihusishwa na maelfu ya watoto wanaozaliwa wakiwa na vichwa vidogo.
tahadhari ya WHO kuhusu Zika ni ya hali ya juu sawa na ya Ebola
hii inamaanisha kuwa utafiti na msaada itatolewa kwa haraka kupambana na maambukizi.
Mkurugenzi mkuu wa WHO, Margaret Chan amesema nguvu ya pamoja inahitajika kupambana na virusi hivyo
amesema masuala yanayopewa kipaumbele ni kuwalinda wanawake wajawazito na Watoto dhidi ya mbu wanaosambaza virusi.
Tangu mwezi Oktoba kumekuwa na ripoti ya kesi 4,000 za watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo nchini Brazil pekee.

Ripoti iliyotufikia kuhusu kipindupindu Tanzania tangu kilivyoanza 2015..


Kumekuwa na ripoti kila siku zikibeba vichwa vya habari Tanzania kuhusu ugonjwa wa kpindupindu, ripoti ya leo imetoka Wizara ya Afya kuhusu idadi ya waliowahi kuugua ugonjwa huo, waliofariki na pia rekodi zinavyoonesha maambukizi kwa sasa.
Ripoti hiyo inaonesha jumla ya watu 15,067 wameugua kipindupindu Tanzania toka ugonjwa huo ulipoanza mwaka 2015, waliofariki ni watu 233 huku mikoa ya Simiyu na Mwanza ikionekana kuongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi kwa wiki hii.

Afande Sele Atoa Wosia....Asema Akifa Achomwe Moto Badala ya Kuzikwa

         Msanii Afande Sele ambaye anawakilisha mkoa wa Morogoro katika muziki amefunguka na kusema kuwa hataki kuja kuwa binadamu tena bali anahitaji kuwa Malaika.

Afande Selle alisema hayo kupitia kipindi cha Planet bongo cha East Africa Radio na kusisitiza kuwa siku atakayo kufa anaomba achomwe moto kwani yeye anaamini katika moto na si kuzikwa kawaida.

Afande Sele alidai kuwa amechoka kuwa binadamu bali anataka kuwa Malaika ndio maana anahitaji kuchomwa moto ili siku ya ufufuo arudi kama Malaika na si binadamu, imani yake inamtuma kuwa akizikwa kwenye udongo siku ya ufufuo atarudi kuwa binadamu tena jambo ambalo yeye hataki kusilisikia tena.

Kufuatia imani hiyo Afande Sele amesema mpaka sasa ameacha wosia kuwa siku atakayokufa achomwe moto na si kuzikwa.

Tazama kwa kifupi kilichotokea ndani ya usiku wa Diva


Usiku wa Diva wafana ndani ya GR City,Mbeya.



Katika kuumaliza ule mwezi ambao watu wengi huuita mwezi dume,yaani Januari..Tarehe 30/01/2016 katika ukumbi wa GR City Hotel,msanii wa filamu mbeya Esther Peter alimaarufu kama Divah alikuwa anaizindua filamu aliyoshiriki nje ya mkoa wa Mbeya,inayojulikana kama ''Kizito'' ambayo iliwabeba wasanii wakubwa kama Lutwaza,Ben na Riyama Ally.Divah aliungwa mkono na wasanii wengine wa kutoka mkoani Mbeya wakiwemo Idrissa,Kelvin 'Tozi' Kaziyandege,Beatrice 'Trice' Kaizaly,Issah 'Bonge la bwana' Ngoda,Peace Salatiel  na wengine wengi wanao fanya vizuri kwenye tasnia hiyo filamu. 
Diva(Katikati) akiwa na baadhi ya wasanii wa Muziki waliokuwepo siku hiyo.
    
  Pia kwa upande wa muziki wali'perform' baadhi ya wasanii ambao ni D-Twice,Nyota,Maridadi na D-Bway. Ma'producer' wa Muziki kama vile Gachi na wengine wengi hawakusahaulika.
Katika kuunga mkono ufanyikaji wa tukio hili Prince Hekela,Binno 'the Genius' na Tom Johns ambao ni ma'director' wa filamu ndani ya Mbeya walihudhuria usiku huu.
 
D-Bway(Kushoto)akiwa na moja ya watu mashuhuri waliokuwepo siku hiyo.

 
D-Twice akiwa anatoa burudani usiku huo
©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved