Polisi Yapiga Marufuku maandamano ya vijana wa Chadema kwenda Ikulu Kesho





 Jeshi la Polisi limetoa tamko kuhusu tangazo la Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) kuwa kesho wamepanga kufanya maandamano hadi Ikulu kwa lengo la kuishinikiza serikali kubadili msimamo wake kuhusu TBC kutorusha Live baadhi ya vikao vya Bunge.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro amepiga marufuku maandamano hayo na kuwataka vijana hao kutumia njia mbadala za kupata ufumbuzi wa suala hilo badala ya maandamano.

Akitoa sababu za kuzuia kufanyika kwa maandamano hayo, Kamanda Sirro alisema kuwa hakuna taarifa  na pia hakuna uthibitisho kuwa maandamano hayo yatapokewa na Rais Magufuli.

Pia, Kamanda Sirro alieleza kuwa BAVICHA hawakuanisha barabara ambazo wanatarajia kutumia katika maandamano hayo.

“Siku hiyo sio nzuri sana kwa sababu ni siku ambayo watu wanakuwa kazini. Ni siku ambayo wengi watataka kutumia barabara hizo kwa ajili ya huduma za kijamii. Na kwa sababu kuna option nyingine ya kuweza kupata suluhu hiyo, nisema tu kwamba maandamano hayo yamepigwa marufuku,” alisema.

WATU 6 WATIWA MBARONI KUFUATIA KUTUNGUIWA HELKOPTA MEATU

Watu sita wanaodaiwa kuwa majangili, wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuitungua helikopta ya doria na kusababisha kifo cha rubani wake katika pori la akiba la Maswa.
Kukamatwa kwa watu hao kumekuja siku moja baada ya Rais, John Magufuli, kutoa agizo kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuwakamatwa waliohusika na tukio hilo na kufikishwa katika mkono ya sheria.
Kauli hiyo ya Rais iliyotolewa  na  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa,  ilisema Rais Magufuli mbali na kusikitishwa na tukio hilo, pia aliuakikisha umma kuwa serikali itahakikisha inaendeleza mapambano dhidi ya ujangili kwa nguvu zote na kuwataka wananchi na wadau mbalimbali wa hifadhi ya wanyamapori kutokatishwa tama.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Gemini Mushy, jana alithibitisha  kukamatwa kwa watu hao.
Alisema awali walikamata watu wawili, juzi watatu na jana mmoja wote wakiwa wakazi wa Simiyu na uchunguzi bado unaendelea.
Ijumaa iliyopita, watu wasiojulikana, waliitungua helikopta hiyo  wakati ikifanya doria katika pori hilo baada ya kuwapo taarifa kwamba majangili walikuwa wameua tembo mmoja.


Katika tukio hilo, rubani wa helikopta hiyo raia wa Uingereza, Rodgers Gower (37) alikufa, huku mwenzake Nicky Bester wa Afrika Kusini akinusurika.

Dogo mwenye umri wa miaka 15 aliyeingia kwenye headlines za kusomea udaktari Afrika Kusini …


Kwa kawaida tumezoea kuona watoto wenye umri wa miaka 15 kuwaona wakiwa elimu ya sekondari hii, imekuwa tofauti kwa mtoto huyu kutoka Thulamahashe Mpumalanga Afrika Kusini kujiunga na chuo cha medicine nchini humo. Mwanafunzi huyo aliyefahamika kwa jina la Decent Junior Mkhombo amejiunga na wanafunzi  wenzake kwenye chuo hiko kilichofunguliwa  mwaka huu nchini Afrika Kusini kwa lengo la kusomea medicine katika chuo hiko cha  University of Limpopo (UL).
Serikali nchini humo imetenga zaidi ya billion 1.3 kwa ajili ya  masomo ya wanafunzi wote wanaotarajiwa kujiunga na chuo hiko, ambao baadae watasaidia matatizo ya afya nchini humo. Decent Junior Mkhombo amekuwa mwanafunzi mwenye umri mdogo nchini humo kusomea udaktari lakini mwaka 2014  Dr.Sandile Kubheka alikuwa mwanafunzi wa kwanza kufuzu mafunzo ya udaktari nchini humo akiwa na umri wa miaka 21
Junior-Mkhombo
Junior Mkhombo akiwa darasani na wanafunzi wenzake
“Nina mapenzi ya kujifunza oncology  kwa sababu kansa ni ugonjwa mkubwa sana na unatakiwa kupatiwa tiba, kikukweli hatuna maktaba, tuna mahabara kwa jina lakini haina vitendea kazi vya kukidhi, lakini tuna waalimu wazuri kama Mr  Richard Walusimbi ambaye amekuwa akitaka tujitume siku zote” >>> Mkhombo

Wabunge Wa Upinzani Wagoma Kuteua Wenyeviti PAC Na LAAC


Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema kutokana na Spika wa Bunge kuteua kibaguzi wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge, wabunge wa upinzani hawatashiriki uchaguzi wa wenyeviti wa kamati mbili ambazo zinapaswa kuongozwa na upinzani.

Amedai kuwa katika kamati hizo za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Mashirika ya Umma (LAAC), wameteuliwa wabunge wa upinzani ambao hawana uwezo mkubwa katika kutekeleza majukumu hayo na wamekataa kabisa kumhamisha na kumuweka Freeman Mbowe kuwa mjumbe wa kamati hizo.
Kwa mujibu wa Tundu Lissu,  ili Mbowe aweze kuwa mwenyekiti wa PAC au LAAC ni lazima awe mjumbe wake, jambo ambalo limekuwa gumu baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kukataa kumpeleka huko.
Tundu Lissu amesema Ndugai amefanya hivyo kwa madai kwamba amepokea amri kutoka mamlaka za juu  asihamishe mjumbe wa kamati zozote ambazo zimetangazwa

Amesema endapo hawataafikiana na Spika na kufanya marekebisho ya wajumbe wa kamati kama wanavyotaka, kamwe hawatakuwa tayari kuongoza kamati hizo

“Hili Bunge litakuwa la vichekesho, maana unasema kamati za usimamizi wa fedha za umma zitaongozwa na wapinzani halafu unawachagulia nani aongoze hizo kamati. Hatushiriki uchaguzi acha waendelee.”

“Kwa mujibu wa mabunge ya jumuiya za madola, kamati hizo mbili lazima ziongozwe na wabunge kutoka upinzani, hivyo majukumu ya PAC hayawezi kuhamishiwa PIC (kamati mpya ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma).”

Mara baada ya Spika kutangaza majina ya Kamati za Kudumu za Bunge, wabunge wa upinzani walipinga jinsi uteuzi huo ulivyofanyika kwa maelezo kuwa wabunge wenye weledi mkubwa walipangiwa kamati zisizojihusisha na masuala makubwa ya kitaifa.

Akizungumzia suala hilo, Naibu Katibu wa Bunge, John Joel alisema kamati hizo zinaweza kuendelea na kazi bila kuwa na wenyeviti.

“Kiutaratibu mwenyekiti wa kamati hizo mbili lazima atoke upinzani ila makamu wake hutokea CCM. Hata wasiposhiriki zitaendelea na kazi chini ya makamu mwenyekiti. Hakuna kanuni inayoeleza kuwa lazima kamati iwe na mwenyekiti. Ni kama bungeni asipokuwepo Spika, shughuli zitaendelea kufanywa na Naibu Spika,” alisema.
Golikipa mahiri wa zamani wa klabu ya Simba Juma Kaseja ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya, bado ana historia nzuri na kubwa ndani ya klabu ya Simba, kwani ni miongoni mwa magolikipa mahiri waliowahi kuidakia timu hiyo kwa mafanikio.
Kama ambavyo wengi hufahamu mtu akifanya vizuri ni lazima apongezwe Juma Kaseja usiku wa February 1 kupitia account yake ya instagram ameandika ujumbe ambao kwa mara moja ni ngumu kuelewa kamaanisha nini, Kaseja katika account yake ya instagram kaandika Wana ssc nikumbukeni kwa mabaya nilio wafanyia kwenye timu yenu mazuri yaacheni”

Diwani Wa CUF Auawa Kwa Kucharangwa Mapanga Na Watu Wasiojulikana

 
Diwani wa kata ya Kimwani iliyoko Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera, Silvester Miga (CUF) amepoteza maisha baada ya kuvamiwa na kukatwa na mapanga nyumbani kwake, usiku wa kuamkia jana.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera, Augustine Ollomi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa marehemu alipoteza maisha majira ya saa saba usiku akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Kagondo.

Imeelezwa kuwa Miga alivamiwa nyumbani kwake akiwa anaangalia taarifa ya habari kwenye runinga ambapo watu hao walimvamia na kutekeleza tukio hilo la kikatili.

Kamanda Ollomi alisema kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo limeendesha msako mkali na kuwakamata watu wawili wanaotuhumiwa kuhusika na tukio hilo.
 Aliwataja watu hao kuwa ni Aderarid Antony mwenye umri wa miaka 42 na Shiranga Gonzari mwenye umri wa miaka 22.

Baadhi ya wakazi wa kata Kimwani waliwaambia waandishi wa habari kuwa mazingira ya kuuawa kwa diwani wao ni ya kisiasa zaidi.
©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved