Sakata La Mauaji Ya Diwani Wa CUF Lachukua Sura Mpya

Mauaji ya kikatili ya Diwani wa Kata ya Kimwani, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Sylvester Muliga (CUF), yameanza kuibua mambo mazito huku ikielezwa kuwa Ijumaa alikuwa awasilishe hoja kwenye Baraza la Madiwani kuhusu masuala ya ardhi.

Muliga ambaye alifia Hospitali ya Kagondo alikopelekwa kwa matibabu baada ya kukatwa mapanga Jumapili usiku, imeelezwa kuwa katika kikao hicho ilikuwa aombe kuundwa kwa kamati ya kuchunguza uhalali wa maeneo makubwa ya ardhi yanayomilikiwa na watu wachache.

Kwa mujibu wa mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Mazingira ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kasharunga, Khalid Swalehe, hoja hiyo ilikuwa iwasilishwe na Muliga na ilikuwa inaungwa mkono na madiwani wa kata zote zilizo na migogoro ya ardhi.

Baada ya taarifa za kufariki dunia kwa diwani huyo, wananchi walivamia nyumba nane za watuhumiwa wanaodaiwa kutekeleza mauaji hayo na kuziteketeza kwa moto.

Pia, walichoma moto mashine mbili za kusaga na kuharibu gari la mmoja wa wagombea wa udiwani katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Kyota, Daudi Kiruma, wananchi wamehusisha mauaji hayo na mambo ya siasa.

“Kinachoonekana hapa baadhi ya watu wanataka kupotosha ajenda ili wahusika wa mauaji wapate nafasi ya kutoroka,” alisema Kiruma.

Hata hivyo, Kiruma alisema hana uhakika kama mtuhumiwa anayedaiwa alikuwa mgombea amekamatwa, kwa sababu haonekani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi, jana alisema wanamshikilia mtuhumiwa mwingine ambaye anafanya idadi ya walikomatwa kuhusiana na mauaji hayo kufikia watatu mpaka sasa.

Kamanda Ollomi aliwataka wananchi wasijadili mauaji hayo kwa hisia za kisiasa bali waviachie vyombo vya dola vifanye kazi yake

Toka Bungeni: Serikali Yakiri Kasoro Mradi wa TASAF...Yaahidi Kufanya Maboresho


Serikali imekiri kuwepo  kasoro nyingi zilizojitokeza katika mradi Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na TASAF ikiwamo ubadhirifu wa fedha kwa Kaya sizizokuwa na sifa kupewa pesa kupitia mpango huo hivyo imejipanga kuborsha zaidi mpango huo katika awamu ya tatu kwa kutengeneza miundombinu mizuri ya kutambua Kaya zinazolengwa.

Akijibu swali la Mhe.Magdalena Hamisi Sakaya Mbunge wa Kaliua (CUF) lililouliza ni vigezo gani vinatumika kuondoa Kaya zilizopendekezwa kwenye mradi na kubakiza Kaya chache, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki amesema mpango wa kunusuru Kaya maskini hutambulishwa kijijini na wataalam kutoka Halmashauri husika kwa kusimamiwa na uongozi wa kijiji kisha kuweka vigezo vya Kaya maskini.

“ Wakusanya taarifa huchaguliwa kutoka miongoni mwa vijana wanaoishi kijijini hapo na kupitia nyumba kwa nyumba kuorodhesha Kaya ambazo zinakidhi vigezo vilivyoanishwa na mkutano wa Kijiji ila bado kuna malalamiko yanayotolewa kuwa Kaya maskini zinaachwa na kupewa Kaya nyingine ambazo sio maskini  
"Kwa kuliona tatizo  suala hili tunalifanyia uchunguzi na tunaomba watu watoe taarifa ikiwa wataona ukiukwaji wa uorodheshaji wa Kaya zitakazohusika na mpango huu ili hatua ziweze kuchukuliwa dhidi ya yoyote atakaye bainika kufanya hivyo

“Mpaka sasa kutokana  na malalamiko yaliyojitokeza katika kuorodhesha Kaya maskini zinazotakiwa kuwezeshwa na mpango huu tumewawajibisha watendaji toka Wilaya za Karagwe, Kagera , kibondo na Kigoma na tuomba kupewa taarifa kwa sehemu yoyote ambapo kutatokea tatizo kama hili na tutachukua hatua mara moja kuokoa fedha zilizotakiwa kwenda kusaidia watu husika” Alisema Mhe Angella Kairuki.

Aidha Mhe. Angella Kairuki ameongeza kuwa kuna taarifa zinazoenezwa kuwa fedha za mpango wa TASAF Awamu ya Tatu ni fedha za freemasons, taarifa hizo sio za kweli kwani fedha hizi zinatolewa na Serikali ili kusaidia Kaya maskini ili ziweze kujikwamua kiuchumi kwa kuweza kupata Elimu Malazi na chakula bora.

TASAF ni mpango wa kunusuru Kaya maskini na imekuwa katika awamu tatu mpaka hadi sasa kwa ajili ya kuwezesha Kaya maskini kujikwamua kiuchumi.

Bungeni: Mbunge Magdalena Sakaya Aituhumu Serikali Kuwa Chanzo Cha Ukosefu Wa Ajira Kwa Vijana

Mbunge wa Jimbo la Kaliua Mkoani Tabora Magdalena Sakaya CUF amesema tatizo kubwa la ajira nchi hii linachangiwa na serikali yenyewe.

Magdalena ameyasema hayo wakati akichangia mpango wa serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ambao uliwasilishwa hapo juzi na wabunge kupewa nafasi ya kuchangia na kuishauri serikali kwa muda wa siku 5.

"Mheshimiwa Naibu Spika nchi hii ni tajiri sana tuna misitu ya kutosha lakini cha kushangaza tunakata miti tunasafirisha kwenda nje kwenda kutengeneza vifaa ambavyo tunakuja kuuziwa kwa bei ya juu wakati vijana nchini hawana ajira wanarandaranda mitaani". Alisema Sakaya na kuomngeza;

"Serikali ndiyo chanzo cha kukosekana kwa ajira kwa vijana nchi hii maana hadi pamba za kusafisha masikio tunatoa nje, pia tumeifanya nchi hii kuwa nchi ya kupokea kila kitu wakati malighafi tunazalisha hapa hapa nchini,Serikali ifufue viwanda ili kuweza kuajiri maelfu ya vijana".

Aidha Mbunge huyo ameitaka serikali kutekeleza kwa vitendo miradi ya maji ambayo iliahidiwa katika wilaya ya Kaliua na kwa muda wote wa mpango uliopita vijiji vitatu tuu ndivyo viliweza kupewa kipaumbele.
Chanzo cha habari Mpekuzi blog

Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi Na Mawasiliano Profesa Mbarawa Amteua Bwana Masanja Kungu Kadogosa Kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Wa TRL

 WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemteua Bwana Masanja Kungu Kadogosa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), ambako anakwenda kuchukua nafasi ya Mhandisi Elias Mshana ambaye anastaafu hivi karibuni.

Kabla ya Uteuzi huo Bwana Masanja Kadogosa alikuwa Mkurugenzi Idara ya Mikopo Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB). Uteuzi huo unaanza mara moja.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
02 Februari, 2016.
Chanzo Mpekuzi blog

WAZIRI WA MAMBO YA NJE AUGUSTINE MAHIGA ALA KIAPO CHA UBUNGE LEO


 Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki na Kikanda, Augustono Mahiga akiapa Bungeni mjini Dodoma Februari 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Naibu Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson akimwapisha Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki na Kikanda, Augustono Mahiga , Bungeni mjini Dodoma Februari 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 

Baraza la Waislam BAKWATA Waunga Mkono Uchaguzi wa Marudio Zanzibar

WAKATI Chama  cha wananchi CUF ambacho ni chama kikuu cha Upinzani visiwani Zanzibar kikiwa kimesusia uchaguzi wa marudio ambao unafanyika Marchi 20 ya mwaka huu,Baraza la Waislam  (BAKWATA)  limesema marudio ya  uchaguzi huo ndo njia ya kipee ya kurudisha amani visiwani humo..

Akizungumza na waandishi wa habari leo,Jijini Dar es Salaam, Sheikh Mkuu mkoani hapa,heikh alhadj Mussa Salum  amesema  Bakwata wanaunga mkono Tangazo la ZEC la kurudiwa kwa uchaguzi hu.

“Uchaguzi huu wa marudio  kwetu Bakwata tunaona ndio njia ya kipekee ya kukiweka kisiwa cha Zanzibar kuwa sehemu ya Amani na utulivu,natumia nafasi hii kuwaomba chama cha CUF kushiriki uchaguzi huu” Amesema Sheikh Salum.

Sheikh Salum ameongeza kwa kusema  kuwa hata kiongozi wa jumuiya ya Uamsho Visiwani Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmad amemwandikia barua na kumweleza kuwa kurudiwa kwa uchaguzi kutasaidia kurudisha Amani visiwani humo.
©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved