Burundi: Uchaguzi utaendelea kama ulivyopangwa
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burundi, Edward Nduwimana, amesema kuwa
uchaguzi wa bunge na ule wa serikali za mitaa utafanyika wiki ijayo kama
ilivyopangwa. Waziri Nduwimana ameashiria hatua ya Umoja wa Ulaya ya
kuwaondoa waangalizi wake na kujiondoa kanisa Katoliki kwenye mchakato
wa uchaguzi na kusema matukio hayo hayawezi kuathiri uchaguzi ujao.
Kiongozi huyo pia amesisitiza kuwa, licha ya maandamano madogo
yanayoendelea Bujumbura, kiujumla hali ni shwari katika maeneo mengi ya
nchi na hivyo kuna mazingira mazuri ya kufanyika uchaguzi juma lijalo.
Edward Nduwimana, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burundi amesema chaguzi
nyingi katika nchi mbalimbali duniani hukumbwa na matatizo ya hapa na
pale na kwa mantiki hiyo, yanayojiri katika nchi yake hayafai kuonekana
kama jambo la ajabu. Uchaguzi wa bunge na serikali za mitaa umepangwa
kufanyika Juni 2.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment