UN: Walinda amani duniani wanakabiliwa na matatizo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moo, amesema kuwa walinda amani
wa umoja huo bado wanakabiliwa na hatari na changamoto nyingi kwenye
kazi zao. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema tangu kuanza mwaka huu
wa 2015, tayari walinda amani 49 wa umoja huo wameuawa katika maeneo
yenye migogoro duniani. Ban Ki-moon pia amesema kuongezeka makundi yenye
misimamo mikali kumeongeza hatari kwa wanajeshi wa kulinda amani kote
duniani. Mwanadiplomasia huyo amesisitiza umuhimu wa kuwanoa zaidi
wanajeshi wa kulinda amani na kuwapa mafunzo na suhula za kisasa ili
waweze kukabiliana na changamoto ibuka. Mkuu huyo wa UN amesisitiza
kuwa, ni vigumu kukabiliana na changamoto za karne ya 21 kwa kutumia
mbinu za karne ya 20.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment