
Mwanasiasa Kijana anayekuja juu katika medani za siasa nchini Tanzania ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha mwigulu Nchemba anatarajia kutangaza nia ya kutaka kugombea urais mwaka 2015.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wake amebainisha kwamba leo siku ya jumapili tarehe Tar.31.05.2015 Nchemba atatangaza nia ya kugombea urais katika na kusisitiza kuwa Mazungumzo yake na wananchi yatajikita katika kuomba ridhaa ndani ya Chama cha Mapinduzi ya Kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, Nchemba atazungumzia nia hiyo majira ya Saa 9 Alasiri hadi 12 Jioni katika ukumbi wa Mwl.Nyerere “Hall “chuo cha Mipango mkoani Dodoma .
Baada ya kuhakikisha kuwa haujapitwa katika tukio la kutangaza nia Mbunge wa Monduli Edward Lowassa leo Team nzima ya Mtandao wa Hivisasa itawasili tena mkoani Dodoma kukujulisha kila kinacho endelea, endelea kuwa nasi.
No comments:
Post a Comment