Viongozi wa Afrika Mashariki kukutana kuijadili Burundi
Viongozi wa jumuiya ya Afrika Mashariki wanakutana hii leo mjini Dar es
Salaam nchini Tanzania kuujadili mgogoro wa Burundi. Chini ya uenyekiti
wa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, viongozi hao kutoka Kenya, Rwanda,
Uganda na Burundi wanakutana kwa mara ya pili mwezi huu kujaribu
kuutafutia ufumbuzi mzozo wa kisiasa wa Burundi ambayo imetumbukia
katika msukosuko baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza atagombea
muhula wa tatu. Uamuzi huo umesababisha maandamano ya umma ambayo
yamedumu kwa miezi miwili na pia yalisababisha jaribio la mapinduzi
lililoshindikana. Na katika kadhia nyingine, naibu wa mkuu wa tume ya
uchaguzi nchini Burundi Spes Caritas Ndironkeye na afisa mwingine wa
tume hiyo wamekimbia nchini na hatma ya uchaguzi wa bunge unaotarajiwa
Ijumaa hii ikiwa haijulikani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment