Wapalestina Gaza wasubiri misaada ya dharura

Wapalestina Gaza wasubiri misaada ya dharuraMamia ya malori yenye misaada ya dharura inaelekea huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Palestina. Mratibu wa misaada ya kibinadamu wa eneo la Ghaza, Ra’ad Futtuh amesema kuwa malori 600 yameingia Ukanda wa Gaza kupitia kivuko cha Karam Abu Salim mapema leo Jumatano. Ra’ad amefafanua kuwa malori 69 yamebeba vifaa vya ujenzi wa nyumba kwa ajili ya miradi ya kimataifa ya kujenga upya nyumba za Wapalestina zilizoharibiwa na Wazayuni wakati wa vita vya siku 50 mwaka uliopita. Pia Ra’ad al-Futtuh amesema malori mengine 150 yamebeba vifaa vya ujenzi wa barabara kwa ajili ya kukarabati barabara zilizoharibiwa kwenye vita hivyo.
Huku hayo yakijiri, ndege za utawala haramu wa Israel zimeshambulia maeneo kadhaa ya Gaza kwa kisingizio cha ulipizaji kisasi baada ya roketi moja kutoka upande wa ukanda huo kuanguka kwenye jangwa upande wa pili. Makundi ya Hamas na Jihadi Islami yamekanusha kurusha roketi yoyote kuelekea Israel.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved