BIDHAA
na maziwa yanayotengenezwa na kampuni ya Asas Dairies Ltd ya mkoani
Iringa kwa mwaka wa tatu mfululizo zimeendelea kushikilia tuzo ya
ubora na kuwa kampuni bora kuliko makapuni mengine ya maziwa hapa
nchini .
Kampuni
hiyo ya Asas Dairies Ltd ambayo ni moja kati ya makampuni ya
kizalendo nchini na moja kati ya makampuni yaliyopata kupewa tuzo ya
ulipaji kodi mzuri na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imeshinda katika
maadhimisho ya wiki ya maziwa mwaka huu tena yaliyofanyika wilaya
Babati mkoani Mara kwa kushindanisha kampuni zaidi ya 20 .
Akizungumzia
ushindi huo afisa masoko wa kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Bw Jimmy
Kiwelu alisema kuwa mbali ya kampuni hiyo kuongoza kwa mwaka huu wa
tatu mfululizo bado bidhaa zake nyingine zimeendelea kushinda
medali mbali mbali na kuonyesha uwezo mkubwa wa kampuni hiyo katika
ubora .
Alisema
baadhi ya makampuni makubwa ambayo yalipata kuingia katika
mashindano hayo ni pamoja na Tanga Fresh, DarFresh,Kilimanjaro
Fresh,Creamer Fresh,Cefa, Grand DeMom ya Engingteng, Nansinya ya Arusha
,Nnronga ya Kilimanjaro mengine mengi. Alisema kuwa bidhaa kwa mwaka huu kila kampuni lilikuwa likishindanisha bidhaa zake tatu huku kampuni yake Asas Dairies Ltd bidhaa zake zote tatu zilishinda na kupewa medali .
Pamoja na kushinda katika bidhaa hizo bado kampuni hiyo ilinyakua tuzo ya jumla katika ubora . Bw Kiwelu
aliwataka watanzania kuendelea kuzipenda bidhaa za Asas Dairies Ltd
kutokana na kuendelea kuongoza katika ubora na kuwa lengo la kampuni
hiyo kuendelea kushinda tuzo za ubora.
Pia
alipongeza watanzania na watumiaji wa bidhaa za Asas Dairies Ltd
kutokana na ushirikiano mkubwa wanaombwa kuihamasisha jamii
kuendelea kutumia maziwa hayo na bidhaa nyingine za chini ya kampuni
ya kizalendo ya Asas Dairies Ltd Bw Kiwelu alisema mwaka huu jumla ya Medali 9 zilikuwa zikishindaniwa ila kampuni Asas Dairies Ltd iliweza kuongoza kushinda medali 3 kati ya 9.
Aliyekuwa mgeni rasmi tena kwa mwaka huu Waziri
wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr. Titus Kamani pamoja na kupongeza
mshindi huyo wa jumla na washiriki wengine katika maonyesho hayo
bado alitaka makampuni zaidi kuendelea kushiriki maonyesho hayo
kwani yanasaidia kutambua changamoto katika utengenezaji wa bidhaa
bora .
Pia
alieleza kufurahishwa na hatua kubwa ya kampuni hiyo ya Asas
Dairies Ltd kwa kuendelea kufanya vizuri katika mashindano hayo ya
ubora wa maziwa nchini na kuwa mbali ya kuwa ni heshima ya kampuni na
mkoa wa Iringa ila bado ni heshima kwa Taifa kuona kamapuni ya ndani
yanaonyesha ufanisi mkubwa katika bidhaa zake .
No comments:
Post a Comment