JACOB Steven Mbura ‘JB’ |
“Kama nilivyoanza kueleza hapo awali kuwa, maisha ya jeshini yalinibadili kwa kiwango kikubwa mno,” aliendelea JB.
“Mikikimikiki ikaendelea kuwa mingi, karibu kila mmoja wetu tulioingia pamoja alikuwa ameshaanza kuyazoea maisha hayo,” anasimulia.
“Mikikimikiki ikaendelea kuwa mingi, karibu kila mmoja wetu tulioingia pamoja alikuwa ameshaanza kuyazoea maisha hayo,” anasimulia.
“Nasimulia
historia hii ya maisha yangu, hususan maisha ya jeshini hakika
nakumbuka mbali sana na wakati mwingine narudisha hisia nyuma na kuyaona
maisha jinsi yanavyobadilika,” alisema JB kwa sauti ya chini huku
akionesha sura ya masikitiko kidogo.
“Mbona
umeonekana kubadilika ghafla kwa kuonesha huzuni namna hii kaka?”
nilimtupia swali hilo wakati nikimsogelea karibu zaidi na kumtazama
machoni bila kuyapepesa macho yangu.(P.T)
“Haaa...,
unajua nakumbuka mbali sana, natamani kukutana mahali fulani na watu
wote ambao tulikuwa pamoja jeshini, natamani tukutane tena pamoja mahali
fulani na tuwe na maisha yale,” alisema mfululizo JB kwa hisia kali
sana huku akiuma kidole kidogo cha mkono wa kulia na kusonya mara nyingi
kwa wakati mmoja.
Hapohapo, napata munkari zaidi wa kujua mengi zaidi kuhusu JB.
Hapohapo, napata munkari zaidi wa kujua mengi zaidi kuhusu JB.
“Kwa ni
nini uwe na shauku ya kukutana na watu uliokuwa nao jeshini tu na si
sehemu nyingine kama shuleni,” nilimuuliza wakati nikiitazama kalamu
yangu kwa umakini kwa kuikagua kama iko ‘fiti’ kudondosha wino
unaotokana na maneno matamu na ya kusisimua kutoka mdomni mwa mfalme
huyu wa filamu kwa sasa, JB katika ubora wake.
“Ni kweli
nimepitia maeneo mengi na kukutana na watu wengi mno tofauti, lakini
kampani ya watu niliokutana nao jeshini, hakika ilikuwa ni zaidi ya
furaha, ucheshi, mshikamano, ushirikiano, kusaidiana na kila aina ya
furaha ya maisha ilipatikana jeshini kwa jamaa niliokuwa....!
JB
anashindwa kumalizia sentensi hiyo, ghafla namuona akisitisha kabisa
mazungumzo, natazama pembeni kidogo, natulia na kisha kumtazama tena.
“Kaka, kaka, kaka, vipi tena,” niliita na kumuuliza nikitarajia huenda angeendelea na simulizi.
Haikuwa hivyo. Nikamuona akiinamisha kichwa katikati ya mapaja yake, na haraka sana akatoa kitambaa chake cha gharama na kujifuta usoni!
Haikuwa hivyo. Nikamuona akiinamisha kichwa katikati ya mapaja yake, na haraka sana akatoa kitambaa chake cha gharama na kujifuta usoni!
Ni hapo
ndipo niligundua kuwa JB alikuwa akidondosha machozi. Ndiyo, tena
machozi ya hisia kali, jambo lililonifanya nibaki nimeduwaa! Alikuwa
akilia! Akiyalilia maisha ya jeshini!
“JB mbona unalia sasa?” nilimuuliza.
“JB mbona unalia sasa?” nilimuuliza.
“Acha tu
mdogo wangu, kama kuna mtu niliyekuwa naye jeshini huko Kabuku Tanga kwa
wakati huo na atabahatika kusoma gazetini simulizi yangu kwa maisha ya
jeshini, atakuwa shahidi wa nilichokisema, yalikuwa ni maisha ambayo
tangu hapo sijawahi kukutana nayo maishani tena, na sijui kama
nitakutana nayo tena,” anabainisha JB na kuendelea kujifuta machoni
huku!
“Kwa sasa
wengine wapo, tena ni viongozi wa ngazi za juu mno serikalini, lakini
kuna waliokwisha tangulia mbele ya haki, maisha yamebadilika sana na
nikuambie kitu mdogo wangu?” anasema JB na kisha kunitupia swali hilo.
Wakati najiandaa kumjibu, namuona aki...
Wakati najiandaa kumjibu, namuona aki...
No comments:
Post a Comment