MKURUGENZI wa Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Walter
De Gregorio, amefutwa kazi baada ya kutoa maneno yenye utani kuhusu
shirikisho hilo kwenye televisheni ya Uswisi.
Gregorio alizungumza kwenye kipindi cha Schawinski kuwa: “Rais wa Fifa,
Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Mawasiliano wote wanasafiri kwenye gari.
Nani ni dereva? Jibu ni polisi.”
Fifa imetangaza jana kwenye taarifa yao kuwa De Gregorio ameamua “kuachia madaraka kwenye ofisi yake”.
Lakini inaaminika ya kuwa aliambiwa ajiuzulu na Rais wa Fifa, Sepp
Blatter na katika taarifa hiyo imeeleza kuwa De Gregorio atabakia Fifa
kama mshauri hadi mwishoni mwa mwaka huu.
Blatter yeye alitangaza ataachia ngazi kuongoza taasisi hiyo mwanzoni
mwa mwezi huu kutokana na kashfa kubwa ya rushwa inayoiandama Fifa na
sasa uchaguzi mwingine utafanyika kati ya Desemba na Februari mwakani.
De Gregorio, 50, amedumu kwenye wadhifa huo tangu Septemba, 2011 na
amekuwa mtu wa karibu sana wa Blatter tangu achukue majukumu hayo na
inaelezwa Blatter hakufurahishwa na ma
No comments:
Post a Comment