Katika michuano hiyo inayoendelea kwenye uwanja wa Twalipo, Chui walitawala mpira huo na kuishinda AFC kwa pointi 55-45. Aidha, timu ya netiboli ya wanawake ya Ngome walitawala mpira na kuwapelekesha AFC kwa mabao 52-5.
Kocha wa kikapu Leonard Kwale aliliambia gazeti hili jana kuwa mchuano wa kuwapata wachezaji bora wa mchezo huo bado ni mrefu, kwani wana kazi ya kuhakikisha hawafanyi uchaguzi wa kimakosa.
Alisema wamedhamiria kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika Mashariki hivyo ni lazima wawe makini kwa kuchagua wachezaji wenye uwezo na wanaojituma.
Kocha wa Ngome, Grace Peter alisema siri ya kuwabana wapinzani wao na kundoka na ushindi huo ni kwa vile timu hiyo ilifanya maandalizi ya muda mrefu.
Alisema kilichowagharimu wapinzani wao kushindwa kutamba mbele yao ni kwa vile kikosi hicho hakina uzoefu wa kutosha kwani kina wachezaji wengi vijana ambao ndio kwanza wanaanza kushiriki michuano hiyo.
Kwa upande wa mpira wa miguu timu ya Nyuki na MMN zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya bao 1-1. Mabao hayo yalifungwa na Amri Mwishehe dakika za kwanza za mchezo huo na Ismail Sheikh.
No comments:
Post a Comment