Mkurugenzi Mkuu wa NIMR Dk. Mwele Malecela |
Dk Mwele ambaye aliwasili wilayani Babati Jumatano wiki hii, kwa ajili ya kupata wadhamini katika wilaya hiyo alikwamishwa na Katibu wa CCM wilayani humo, Daniel ole Parokwa ambaye hakuwepo ofisini.
Akizungumza na gazeti hili akiwa jijini Arusha, Dk Mwele alisema aliwasili Babati tangu mchana na tayari alikuta wadhamini wakimsubiri, lakini alimkosa katibu huyo ofisini na alipompigia simu yake ya kiganjani, iliita mara kadhaa bila kupokewa.
Dk Mwele alidai kuwa katibu huyo alikuwa na taarifa kuwa angefika ofisini hapo kupata wadhamini, lakini cha kusikitisha Ole Parokwa hakupokea simu yake hadi ilipofika saa 12 jioni huku akimjibu kuwa muda wa kufanya kazi za ofisiumekwisha.
Kutokana na majibu hayo, Dk Mwele alisema alilazimika kulala Babati na kusubiri hadi kesho yake asubuhi na kwenda tena katika ofisi hizo za chama na kumkuta katibu huyo na kumuomba amsainie fomu yake na ndipo ikasainiwa.
Dk Mwele alionesha kusikitishwa na kitendo cha katibu huyo na kudai kuwa makao makuu ya CCM Taifa walishatuma taarifa kwenye ofisi za CCM za mikoa yote na wilaya zote kuwa wagombea urais watapita kwenye wilaya zao kwa ajili ya kupata udhamini na hajui kwa nini katibu huyo hakuwepo ofisini kwake.
Akizungumzia sakata hilo kupitia simu yake ya kiganjani, Ole Parokwa alisema mgombea huyo alipaswa kutoa taarifa mapema kabla ya kufika ofisini kwake, lakini cha kushangaza alipiga simu saa 11;45 jioni nje ya muda wa kazi.
Wakati huo kwa mujibu wa Ole Parokwa, alikuwa katika tawi la Nangarakati kutafuta wadhamini.
No comments:
Post a Comment