G7 kuanza mkutano wa kilele
Mataifa saba yenye nguvu za kiuchumi duniani, G7, yanaanza mkutano wao
wa kilele hivi leo katika kijiji cha Elmau kusini mwa Ujerumani, huku
mzozo wa madeni wa Ugiriki ukizidi kuja juu. Jana Kansela Angela Merkel
wa Ujerumani alizungumza kwa njia ya simu na Rais Francoise Hollande wa
Ufaransa na Waziri Mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras, kujadili deni la
Ugiriki, wakati muda wa mwisho wa kufikia makubaliano juu ya deni hilo
ukiwadia. Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Jean-Claude Juncker,
alikataa kuzungumza kwa simu na Tsipras hapo jana, akisema hakuna
maendeleo yoyote yaliyofikiwa kwa upande wa Ugiriki. Juzi Ijumaa,
Tsipras aliwataka wakopeshaji wa nchi yake kuondoa masharti aliyoyaita
"ya kuudhi" ili pande hizo mbili zifikie makubaliano. Uwezekano wa
Ugiriki kutangazwa muflisi unautishia mustakabal wa sarafu ya euro.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment