Upinzani Burundi wataka uchaguzi wa rais kabla ya Agosti
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Burundi amesema kuwa lazima uchaguzi wa
rais ufanyike mwezi wa nane mwaka huu, ingawa amekiri kuwa hakuna
uwezekano wa uchaguzi huo kuwa huru na wa haki bila ya usalama na vyombo
huru vya habari. Agathon Rwasa anayegombea urais dhidi ya rais wa sasa,
Pierre Nkurunziza, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba
kufikia Agosti mwaka huu muhula wa mwisho wa Rais Nkurunziza unamalizika
na ni vyema uchaguzi ukawa umeshafanyika. Rwasa amesema hakuna
uwezekano wowote wa kuwa na serikali ya mpito na kwamba lazima katiba
iheshimiwe. Maandamano ya siku kadhaa yaliyofuatiwa na jaribio
lililoshindwa la mapinduzi yalichochewa na uamuzi wa Rais Nkurunziza wa
kuendelea kugombea muhula wa tatu, hatua ambayo wapinzani wake wanasema
inakiuka katiba na makubaliano ya amani ya Arusha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment