G7 yatangaza mikakati ya kuinusuru dunia

Mkutano wa nchi tajiri za kiviwanda G7, umetangaza mikakati ya kuondosha gesi chafu ya sumu na kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi. Viongozi wa nchi hizo wamekubaliana hitaji la kuendeleza uzalishaji wa nishati ya umeme mbadala na ule utokanao na nguvu za nyuklia ifikapo mwaka 2050, na kuongeza kuwa kufikia mwisho wa karne, mafuta yatokayo na madini ya fosil hayatounguzwa katika sekta yoyote ya uchumi.
Viongozi hao pia wamekubali kwamba nchi tajiri zinapaswa kuzisaidia nchi masikini haswa barani Afrika, kuendeleza teknolojia safi na kukubali mabadiliko ya tabia nchi ambayo hayaepukiki.
Mwandishi wa BBC wa maswala ya mazingira ameyaelezea makubaliano hayo kama ni kuhama katika matetemeko ya ardhi. Ameongeza kuwa matokeo chanya ya mpango wa dunia yaliyofikiwa kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabia ya nchi uliofanyika mjini Paris mwezi Desemba, sasa yaonekana kudhihirika zaidi.
Kansla wa Ujeruman Angela Merkel, amesema viongozi wa nchi zinazounda kundi la G7 wamekubaliana kufuata hatua mbalimbali ili kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.(VICTOR)
Akizungumza baada ya mjadala huo, Merkel amesema kwamba kulikuwa na makubaliano ya kuendeleza ongezeko la joto kwa nyuzi joto mbili ya nchi ambazo hazijakuwa kiviwanda.
Kansela Angela Merkel na rais wa Nigeria BuhariMerkel ameongeza kuwa, suala hili lingejadiliwa kwa kiwango kikubwa kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi wa umoja wa mataifa mwezi Disemba huko mjini Paris.
"tunataka kanuni zenye nguvu katika makubaliano. Hatuna kanuni zenye nguvu kwa sasa ndio maana hilo litakuwa agenda huko mjini Paris.Tunataka kuhakikisha kwamba nchi zote zipo kwenye nafasi ya maendeleo ili wastani wa joto iwe chini ya digrii mbili. Kwa maneno mengine ni kwamba makubaliano yatahusu mjadala kuhusu digrii mbili. Unajua swala hili litamaanisha kupungua hewa ya sumu duniani kote, na tumekubali kwa namna kwamba katika mwendo wa karne hii tunataka kuona na tunahitaji kuondoa gesi ya kabon ya uchumi wa dunia" alisema Merkel.
Kwa upande wake rais Barack Obama amesema, mapambano dhidi ya wanamgambo wa Islamic State yatafanyika kwa kiwango kikubwa nchini Iraq.
Akizungumza katika mkutano huo, rais Obama ameelezea umuhimu wa kuwashirikisha waislamu wa Sunni kwenye mapambano dhidi ya I-S katika kiini chake, huku akisema kuwa uvamizi wa kijeshi unapaswa kwenda sambamba na siasa

.CHANZO:BBC

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved